Orodha ya wapiga gitaa wa Afrika
Hii ni orodha ya wapiga gitaa maarufu barani Afrika.
Kialfabeti
hariri- Barthelemy Attisso - mpigaji gitaa kiongozi wa bendi ya Orchestre Baobab, huko nchini Senegal.
- Omara "Bombino" Moctar - mpigaji maarufu, mwimbaji na mtunzi kutoka mjini Agadez, Niger.
- Alick Macheso - mpigaji gitaa mkuu wa bendi ya Orchestra Mberikwazvo, nchini Zimbabwe.
- Oliver De Coque - wa Ogene Sound Super of Africa
- Mamadou Diop (pia anajulikana kama Modou Diop) - mpiga rizim gitaa wa kutoka Senegal, lakini kwa sasa yupo nchini Marekani
- Afel Bocoum - Mpiga gitaa marufu kutoka nchini Mali, Ali Farka Touré ndiye mwalimu wake
- Henri Bowane - Ni mtu mkubwa katika masuala mazima ya uanzishwaji wa rumba la Kikongo, wanafunzi wa awali wa Franco.
- Diblo Dibala - Mwanamuziki wa Kikongo ambaye maarufu kwa mtindo wa soukous, anafahamika kama "Machine Gun" kwa kasi na maarifa yke ya juu katika upigaji mzima wa gitaa.
- Nico Kasanda (aka "Dr. Nico") - mmoja kati ya waanzilishi wa muziki wa soukous.
- François Luambo Makiadi (aka "Franco") - Mwanamuziki wa Kikongo, mwanzilishi wa kundi zima la muziki wa Jazz maarufu OK Jazz.
- Nico Mbarga - mpigaji gitaa mkuu na mtunzi maarufu wa wimbo maarufu wa "Sweet Mother."
- Oliver Mtukudzi - Mpigaji gitaa kutoka nchini Zimbabwe na kiongozi wa 'Black Spirits'
- Jean-Bosco Mwenda - Mwanzilishi wa mtindo wa Kiafrika maarufu "mtindo wa kidole" katika miaka ya 1950, Kongo
- Ray Phiri- Mpigaji gitaa marufu kutoka mjini Mpumalanga, Afrika Kusini
- Jonah Sithole Mpigaji gitaa kutoka nchini Zimbabwe, anapiga na Thomas Mapfumo
- Djelimady Tounkara, mpiga gitaa maarufu wa bendi ya Super Rail Band kutoka mjini Bamako, Mali.
- Ali Farka Touré - mwimbaji na mpiga gitaa kutoka nchini Mali.
- Vieux Farka Touré - mtoto wa Ali Farka Touré, anachipukia kutoka nchini Mali.
- Sir Victor Uwaifo- Mpigaji gitaa kutoka kwa watu wanaongea Kibini/Kiedo, yupo mjini Benin, Jimbo la Edo, Nigeria.
- Dr Sir Warrior - Mwimbaji na Mpigaji gitaa wa bendi ya Oriental Brothers International Band
- Jonah Sithole - Mpiga mbira na gitaa marehemu ambaye awali alikuwa anapiga na Thomas Mapfumo
- Joshua Dube - Mpigaji gitaa hayati ambaye awali alikuwa akipiga na Thomas Mapfumo
- Habib Koité - mwimbaji na mpigaji gitaa kutoka nchini Senegal