Palamagamba Kabudi

Mwanasiasa wa Tanzania

Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (alizaliwa 24 Februari 1956) ni mwanasheria wa Tanzania aliyewahi kuwa waziri.

Palamagamba Kabudi mwaka 2019

Maisha ya Awali na Elimu

Kabudi alizaliwa katika mkoa wa Singida, alisoma katika shule ya msingi Kilimatinde kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1965; mwaka 1966 alihamia shule ya Kitete Primary school, na mwaka 1967 alihamia shule ya Berega Primary School.

Mwaka 1971 alijiunga na shule ya upili ya Tosamaganga alipomaliza kidato cha 6 mnamo 1974. Kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisoma sheria hadi kuhitimu na shahada ya uzamili mnamo 1986. 1989 hadi 1995 alisoma Berlin, Ujerumani akapokea shahada ya uzamili (PhD) ya sheria [1]

Alikuwa profesa ya sheria kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hadi mwaka 2017 alipoitwa na rais Magufuli kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa waziri wa sheria.[2] Mwaka 2019 alibadilishwa kazi kuwa waziri wa mambo ya nje. Mwaka 2021 alipangwa tena wizara ya sheria na katiba[3].

Kwenye Januari 2022 Kabudi alitoka katika uwaziri akapewa nafasi ya mshauri katika Ofisi ya Rais.[4]

Marejeo

  1. profile Hon. Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, tovuti ya Bune la Tanzania, iliangaliwa machi 2021
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-24. Iliwekwa mnamo 2021-02-18.
  3. Rais Samia afanya mabadiliko baraza la mawaziri, Mwananchi 31.03.2014
  4. "President Samia: Why I dropped Kabudi and Lukuvi". The Citizen (kwa Kiingereza). 2022-01-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-15. Iliwekwa mnamo 2022-01-15. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)