Pangaia

(Elekezwa kutoka Pangaea)

Pangaia (pia: Pangaea kutoka Kigiriki πᾶν pan "yote" na γαῖα gaia ardhi, dunia) ni neno linalomaanisha "dunia yote, dunia nzima".

Ramani ya Pangaia inayoonesha vipande vyake viliovyokuwa mabara ya leo
Mwendo wa mabamba: jinsi Pangaea ilivyoachana na mabara ya leo kutokea

Katika nadharia ya sayansi ya jiografia inamaanisha bara kubwa linaloaminiwa kuwa liliunganisha mabara yote ya dunia ya leo takriban miaka milioni 250 iliyopita. Maana yake wakati ule sehemu zote za nchi kavu zilikuwepo mahali pamoja kwenye uso wa dunia yetu. Bara hilo kuu lilizungukwa na maji ya Panthalassa iliyokuwa bahari pekee duniani.

Kusambaratika kwa Pangaia

hariri

Kutokana na mwendo wa gandunia Pangaia ilianza kuvunjika takriban miaka milioni 150 iliyopita. Sehemu kubwa 2 zinazoitwa na wataalamu Laurasia na Gondwana zikatokea ambazo zikaendelea kuvunjika tena kwa mabamba ya gandunia ambayo leo hii ni mabara tunavyoyajua.

Pangaia ya nadharia ya gandunia

hariri

Katika mawazo ya wataalamu Pangaia haikuwa bara la kwanza duniani; yenyewe ilitokea baada ya kugongana kwa mabara yaliyotangulia. Katika nadharia ya gandunia kila bara liko kwenye bamba la gandunia linaloelea juu ya magma moto ya koti ya dunia. Joto la magma linasukuma mabamba hayo na kusababisha mwendo wa mabamba yanayoweza kukaribiana hadi kuungana au kuvunjia na kwenda mbali.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.