Pango la Denisova
Pango la Denisova (kwa Kirusi: Денисова пещера, Denísova peshchéra) linapatikana katika milima ya Altai, Siberia, Urusi.
Ni muhimu katika utafiti juu ya asili ya binadamu kutokana na upatikanaji wa mabaki ya aina mbalimbali za viumbehai wa jenasi Homo. Aina mojawapo imepewa jina la pango hilo (Denisova hominin au Homo denisova), nyingine ni maarufu kama Homo neanderthaliensis, mbali ya Homo sapiens sapiens[1].
Mabaki hayo yanaonekana kuthibitisha kwamba aina hizo zilizaliana.
Tanbihi
hariri- ↑ The Siberian Times reporter, Homo sapiens or Denisovans? Who made stunning cave jewellery and artefacts up to 48,000 years ago?, The Siberian Times, February 4, 2016
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Pango la Denisova kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |