Paraguay (mto)
Mto wa Paraguay ni tawimto mkubwa wa Rio Paraná. Jina laandikwa katika Brazil kwa Kireno "Rio Paraguai", baadaye nchini Paraguay kwa Kihispania "Río Paraguay".
Chanzo | nyanda za juu za Mato Grosso (Brazil) |
Mdomo | mto wa Parana |
Nchi | Brazil, Bolivia (kilomita chache), Paraguay Argentina |
Urefu | 2,625 km |
Mkondo | 4,300 m³/s |
Eneo la beseni | 1,200,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Caceres, Corumba, Asuncion |
Mto unaanza Brazil katika nyanda za juu za Mato Grosso 1154 km kaskazini ya Cuiabá ukielekea kusini. Baada ya kutoka katika nyanda za juu mto unapita tambarare ya Pantanal hapi ni mpaka kati ya Brazil na Bolivia.
Mto hukata Paraguay yote hadi Asuncion na kuingia Argentina. Unaishia kwenye Rio Parana karibu na Corrientes.
Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Paraguay (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |