Bolivia (jina linatokana na shujaa Simon Bolivar) ni nchi isiyo na mwambao wa bahari katika Amerika Kusini.

República de Bolivia
Jamhuri ya Bolivia
Bendera ya Bolivia Nembo ya Bolivia
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Kihispania: ¡Morir antes que esclavos vivir!
("Heri kufa kuliko kuishi kama watumwa")
Wimbo wa taifa: Bolivianos, el hado propicio
Lokeshen ya Bolivia
Mji mkuu Sucre
16°29′ S 68°8′ W
Mji mkubwa nchini Santa Cruz
Lugha rasmi Kihispania, Kiguarani, Kiquechua, Kiaymara
Serikali Jamhuri
Luis Arce
Uhuru
Kutoka Hispania
6 Agosti 1825
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,098,581 km² (ya 28)
1.29%
Idadi ya watu
 - 25 Machi 2014 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,556,102 (ya 83)
8,280,184
9/km² (ya 221)
Fedha Boliviano (BOB)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
— (UTC-4)
— (UTC?)
Intaneti TLD .bo
Kodi ya simu +591

-


Ramani ya Bolivia
Mji wa La Paz
Uyuni

Imepakana na Brazil, Paraguay, Argentina, Chile na Peru.

Jiografia

hariri

Nchi inakatwa na safu mbili za milima ya Andes zenye kimo hadi mita 6500 juu ya UB.

Nyanda za juu (kwa Kihispania: "Altiplano") zinakaliwa na wakazi wengi (80%) ziko kwenye kimo cha mita 3.000 hadi 4.000. Altiplano ni takriban theluthi moja ya eneo la nchi; sehemu nyingi ni tambarare ya "llanos" ambayo ni nchi ya chini yenye joto ambayo ina sehemu mbili: savana kavu za Gran Chaco na misitu minene ya beseni ya Amazonas.

Ziwa la Titicaca liko kwenye Altiplano.

Bolivia ni kati ya nchi maskini zaidi za Amerika Kusini.

Tofauti na nchi nyingine za bara hilo, wakazi asilia (Waindio) ni sehemu kubwa ya wananchi (55%), wakifuatwa na machotara (30%) na watu wenye asili ya Ulaya (15%).

Lugha rasmi ziko 37, kuanzia Kihispania na lugha nyingi asilia.

Upande wa dini, Kanisa Katoliki linaongoza (78%), likifuatwa na Uprotestanti (19%).

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

  Makala hii kuhusu maeneo ya Bolivia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bolivia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.