Paul Kibii Tergat (amezaliwa Riwo, kaunti ya Baringo, 17 Juni 1969) ni mwanariadha maarufu kutoka nchini Kenya. Yeye alishikilia rekodi ya Marathoni tangu mwaka wa 2003 hadi 2007, akiwa amekimbia kwa muda wa 2:04:55, na anaonekana kama mmoja kati ya wakimbiaji bora wa muda wote.

Mwanariadha maarufu wa KenyaKenya

Katika hali ya kuzingatia mbio ya masafa marefu tu, Tergat ameshinda tuzo nyingi na kuweka rekodi kadhaa za dunia kwenye uwanja, kwenye mbio za nchi kavu na hata kwenye barabara ya lami. Alipewa jina la utani la "Gentleman". Tergat ni mtu wa kufanya bidii katika kazi zake na hujipa motisha sana. Yeye huishi na hufanya mazoezi yake ya mbio Ngong, karibu na jiji la Nairobi.

Tergat alishinda tuzo ya mashindano ya IAAF World Cross Country mara tano mfululizo,1995-1999 ambayo ilkuwa rekodi. Tergat alisema, "Mbio za nchi kavu ndizo mimi nilipenda zaidi." Ilikuwa dunia yangu na kitu nilichopenda kabisa. Kabla ya IAAF kuanzisha mbio fupi mwaka wa 1998,wanariadha dunia yote wa daraja tofauti kutoka kwa 1500 hadi wa mbio za masafa marefu walikuwa katika mbio sawa."

Yeye alishinda Mashindano ya mbio ya Lisbon 2000 kwa kuweka rekodi mpya ya mbio hizo na muda bora ya kibinafsi wa 59.06,zote bado zipo hadi mwaka wa 2010. Yeye alishinda mbio hizo tena mwaka wa 2005. Mafanikio ya Tergat pia ni ushindi mara tano katika Mbio ya Barabara za Saint Silvester, mbio muhimu kabisa katika mbio za barabara za Amerika Kusini. Yeye anashikilia rekodi kwa mbio ya umbali wa kilomita 15, ambayo yeye aliiweka mwaka wa 1995. Umaarufu wake katika mbio ya Saint Silvester umempa sifa sana nchini Brazil.

Yeye amekuwa na mashindano makali na rafiki yake Haile Gebrselassie wa Ethiopia. Katika fainali ya mbio ya Olimpiki ya 10,000m Olimpiki ya Atlanta ya 1996 na za Olimpiki ya Sydney ya 2000,alishindwa na Gebrselassie kwa muda mdogo sana. Katika mwaka wa 2000, Gebrselassie alipata ushindi kwa tusui wa sekunde tu.

Tergat alimaliza mbio akiwa wa pili baada ya Gebrselassie katika mwaka wa 1997 na 1999 kwa Mbio ya Mabingwa wa Dunia katika 10,000 m, na kumaliza akiwa wa tatu katika toleo la mbio hizo la 1995 nyuma ya Gebrselassie na Khalid Skah wa Morocco.

Kwenye treki,Tergat alivunja rekodi ya dunia ya Gebrselassie katika mbio ya 10,000m tarehe 22 Agosti 1997 mjini Brussels kwa muda wa dakika 26:27.85. Rekodi hii ilivunjwa tena na Gebrselassie katika mwaka wa 1998 (kwa muda wa dakika 26:22.75), lakini muda wa Tergat unabakia kuwa rekodi nchini Kenya. Tergat akavunja rekodi ya dunia ya mbio ya nusu masafa marefu tarehe 4 Aprili 1998 mjini Milan kwa muda wa dakika 59:17. (Tergat alikuwa amewahi kukimbia kwa dakika 58:51 katika mbio ya nusu masafa marefu za Stramilano nusu marathon mwaka wa 1996, lakini pia ya kuelekeza wanariadha ilikuwa imewekwa vibaya na kuifanya kozi iwe fupi.Hivyo basi,hakuna rekodi iliyokubaliwa kutoka mbio hizo.) Rekodi yake ilipita rekodi ya dakika 59:47 iliyowekwa na Moses Tanui katika mwaka wa 1993. Rekodi yake Tergat ilivunjwa mwaka wa 2005 na Samuel Wanjiru,anayetoka Kenya pia.

Tergat na Gebrselassie walipokimbia katika mbio ya London, Tergat alimshinda Gebrselassie alipochukua nafasi ya pili nyuma ya Khalid Khannouchi. Wanariadha hao watatu walikimbia tena katika toleo la 200z la mbio hizo za London lakini Tergat tu ndiye aliyemaliza kati ya wote watatu.

Wasifu wa Mbio

hariri
 
Paul Tergat,Drew Barrymore na Josette Sheeran Shiner walipokutana na Condoleezza Rice

Tergat alimaliza katika nafasi ya pili katika mbio zake tatu za kwanza: mbio ya London(mwaka wa 2001 na 2002) na mbio ya Chicago(mwaka 2001). Aliendelea kukimbia mbio hizo refu na kuchukua nafasi ya nne mara mbili: mbio ya Chicago (2002) na mbio ya London (2003).

Yeye aliweka rekodi mpya wa muda wa 2:04:55 tarehe 28 Septemba 2003 katika mbio ya Berlin. Hiyo ni kasi ya kilomita moja kwa dakika 0:02:57 yaani kilomita 20.3 kwa kila saa au maili moja kwa dakika 0:04:46. Katika mbio yake aliyovunja nayo rekodi ya dunia , Tergat aliumiza vibaya mguu wake. Baadaye, alisema kuwa alijisikia kama soli ya kiatu ilitoka alipokuwa akikimbia. Yeye ,pia, alipiga kona vibaya alipokuwa akikaribia mwisho wa mbio. Mwanariadha mwenzake kutoka Kenya,Sammy Korir, karibu amfikie. Korir alichukua nafasi ya pili katika muda wa 2:04:56, iliyokuwa muda wa kasi ya pili katika historia ya mbio ya aina hizo.

Rekodi ya dunia ya Tergat ilivunjwa katika mwaka wa 2007 na Haile Gebrselassie wa Ethiopia. Muda huo ulibaki kuwa rekodi ya Kenya hadi mwaka wa 2009,Duncan Kibet na James Kwambai(aliyechukua nafasi ya pili) walikuwa na muda wa 2:04:27 katika mbio ya Rotterdam.

Tergat alishinda mbio ya New York tarehe 6 Novemba 2005 alipotimua mbio kali katika mkondo wa mwisho ili kumshinda Bingwa mtetezi Hendrick Ramaala kwa muda wa 2:09:29.90 kwa 2:09:30.22.

Katika mbio ya Olimpiki ya Athens ya 2004, Tergat alikosa maji yake spesheli alioandaliwa na akanywa maji ambayo hutolewa na waandalizi. Yeye alikuwa amezoea kunywa maji spesheli enye joto la kawaida; waandalizi walipena maji baridi, ambayo yalimtaabisha Tergat. Alihitimu nafasi ya 10 katika mbio hizo.

Mwaka uo huo,Tergat alizindua Mbio ya nusu masafa marefu za Baringo,akiiunda njia ya mbio hizo kupita karibu na mji wake wa nyumbani.

Wiki moja kabla ya mbio ya London 23 Aprili 2006,Tergat alijitoa kwa kuumia misuli ya miguu. Akisema kuwa kuumia huko ni katili kwake,alilazimishwa kujitoa kwenye mbio hiyo iliyokuwa na Haile Gebrselassie. Felix Limo wa Kenya ndiye aiyeshinda mbio hiyo.

Marílson Gomes dos Santos alishinda mbio ya New York ya 2006;huku Tergat akimaliza akiwa nafasi ya tatu. Gomesa aliacha kikundi cha kuongoza katika maili ya 19 lakini Tergat hakumsogea.Tergat alisema baadaye, "Kusema kweli,sikujua yeye ni nani." Tergat alimkaribia Gomes kwa maili tano za mwisho lakini hakumpita.

Tergat alimaliza katika nafasi ya sita (muda wa 2:08:06) katika mbio ya London katika mwezi wa Aprili 2007. Katika mbio hiyo kulikuwa na Haile Gebrselassie wa Ethiopia, ambaye aliacha kukimbia baada ya kilomita 30. Martin Lel wa Kenya ndiye aliyeshinda mbio hiyo katika muda wa 2:07.42, baada ya mbio kali hapo mwisho.

 
Mojawapo wa mashindano kali kati ya Haile Gebrselassie na Paul Tergat

Tarehe 30 Septemba 2007,mwanariadha wa Ethiopia Haile Gebrselassie alivunja rekodi ya Tergat ya muda wa 2:04.55, alipokamilisha mbio ya Berlin katika muda wa 2:04:26. Muda mfupi baada ya kumaliza mbio, Gebrselassie alimwomba Tergat amwie radhi kwa kuvunja rekodi yake(alipopigiwa simu ya kuambiwa hongera na Tergat). Gebrselassie baadaye alielezea, "Niwie radhi - hii ni rekodi ya Paul Tergat," Gebrselassie aliwaambia wanahabari katika mkutano wa habari. "Paulo ni rafiki yangu,"alisema Haile.

Yeye alionyesha azimio la kutaka kushindana katika Olimpiki ya mwaka wa 2008,lakini hakuchaguliwa kuwakilisha Kenya. Alihitimu nafasi ya 4 katika mbio ya mjini New York baadaye katika mwaka wa 2008.

Katika mwaka wa 2009, yeye alishinda mbio ya Lake Biwa katika Ujapani, kwa muda wa 2:10:22. Mnamo Oktoba 2009, yeye alikuwa mgeni rasmi katika kuzindua Mbio ya Belgrad ya Kihistoria. Ingawa hakushinda kamwe mbio zozote kaika miaka ya 1990, alikuwa mshindani pekee kukimbia katika mbio zote nne na kumaliza katika nafasi tatu za kwanza kila mara. Alisema nia yake ilkuwa kufunga kazi yake katika mbio hiyo na akasifiwa njia iliyokuza utamaduni wa Serbia.

1995 Medali ya dhahabu, Mbio ya Dunia ya 1995 IAAF Mabingwa

Medali ya shaba, Mbio ya 1995 ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha (10,000 m)

  • 1996
    • Medali y fedha,Mbio ya Olimpiki ya 1996 (10,000 m)
    • Medali ya fedha, Mbio ya 1997 Mabingwa wa Dunia katika Riadha (10,000 m)
    • Medali ya dhahabu, Mbio ya IAAF ya Dunia ya Mabingwa
    • Medali ya dhahabu, Mbio ya 1999 Mabingwa wa Dunia katika Riadha(10,000 m)
    • Medali ya dhahabu, Mbio ya IAAF World Half Marathon Mabingwa

2000

    • Medali ya shaba,Mbio ya 2000 IAAF World Cross Country ya Mabingwa
    • Medali ya fedha,Mbio ya [Olimpiki ya 2000] (10,000 m)
    • Medali ya dhahabu, Mbio ya IAAF World Half Marathon ya Mabingwa

Ubora wa kibinafsi

hariri

"+" inamaanisha njia hiyo ilikuwa ndefu zaidi ya kawaida
"a" inamaanisha njia ilikuwa kwa mteremko

Umbali Muda aliotumia Tarehe Mahali Alipokimbia
3,000 m 7:28.70 1996-08-10 Monaco
5,000 m 12:49.87 1997-08-13 Zürich
10,000 m 26:27.85 1997-08-22 Brussels
10 km (barabarani) 27:45+ 2006-03-26 Lisbon
15 km (barabarani) 42:04+ 1998-04-04 Milan
Maili kumi (barabarani) 45:12+ 1998-04-04 Milan
20 km (barabarani) 56:18+ 1998-04-04 Milan
Nusu masafa marefu 59:06a 2000-03-26 Lisbon
30 km (barabarani) 1:29:00+ 2002-04-14 London
Masafa marefu 2:04:55 2003-09-28 Berlin

Shughuli nyingine

hariri

Tergat aliteuliwa kuwa "Balozi wa Kupambana na Njaa" na UN Mpango wa Chakula Duniani hapo tarehe Januari 2004. Alipokuwa mtoto, Paul Tergat familia ilikuwa maskini sana hawakuweza kumpeleka shule na chakula. Kulingana Tergat, yeye hangepata elimu kamili kama hakungekuwa na Mpango wa Chakula Duniani, ambayo ilitoa chakula cha mchana katika shule yake.

Tergat alianzisha Paul Tergat Foundation mwaka 2005. Maana ni kuwasaidia yaliyosahaulika Kenya sportspeople [54] Yeye anaendesha kampuni ya kupigia debe michezo na ya kuendeleza mahusiano mema na raiainayojulikana kama Fine Touch Communications (hii huandaa,pamoja na kampuni ya Safaricom, tuzo za michezo na wachezaji wa mwaka zinazojulikana kama tuzo za SOYA) Yeye pia alikuwa akifikiri juu ya kuzindua aina ya nguo zikiwa na jina "Tergat" katika miezi ijayo.

Kama wanariadha wengi wa Kenya, Tergat ni mwanajeshi katika jeshi la Kenya. Makao yake ya jeshi yakiwa Moi Air Base,Nairobi.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri