Monako
Utemi wa Monako (kwa Kifaransa: Principauté de Monaco; kwa Kimonako: Principatu de Munegu) au "Monako" kwa kifupi ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Kuna nchi moja tu ndogo zaidi ambayo ni mji wa Vatikano. Hali halisi ni dola-mji ambako mji ni sawa na nchi na dola lote.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Deo Juvante (kwa Kilatini: Kwa msaada wa Mungu) | |||||
Wimbo wa taifa: Hymne Monégasque | |||||
Mji mkuu | Monaco1 | ||||
Eneo lenye watu wengi | Monte Carlo | ||||
Lugha rasmi | Kifaransa2 | ||||
Serikali | Ufalme wenye katiba (Utemi) Albert II | ||||
Uhuru Watemi wa Grimaldi kukubaliwa na mfalme wa Ufaransa kuwa wanajitegemea |
1489 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
2.02 km² (193rd) 0.0% | ||||
Idadi ya watu - 2011 kadirio - 2008 sensa - Msongamano wa watu |
36,371 (ya 217) 35,352 18,005/km² (ya 1) | ||||
Fedha | Euro (EUR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .mc | ||||
Kodi ya simu | +377
- | ||||
1Monako ni dola-mji. 2Kiitalia hutumiwa pia na wengi |
Eneo
haririEneo lake ni kanda nyembamba ufukoni mwa bahari ya Mediteranea tu, lenye urefu wa kilometa 4 pekee karibu na mpaka wa Ufaransa na Italia, lakini ndani ya eneo lililotwaliwa na Ufaransa mwaka 1859 kutoka Ufalme wa Sardinia.
Baada ya kupata nchi kavu mpya kutoka baharini eneo limeongezeka hekta 42 kuwa 202 au km² 2.02.
Kuna mitaa sita mjini au nchini ndiyo Monte Carlo, La Condamine, Fontvieille, Le Larvotto, Les Moneghetti na Monaco-Ville.
Hakuna nchi yenye msongamano mkubwa duniani kuliko Monako ikiwa na wakazi zaidi ya 18,000 kwa kilomita ya mraba.
Wakazi
haririLugha inayotumika hasa ni Kifaransa ambayo ni lugha rasmi. Sehemu ya wananchi bado hutumia Kimonako ambacho ni lahaja ya lugha ya Kiliguria inayotumika katika mkoa wa Liguria (Italia Kaskazini).
Monako ina dini rasmi ambayo ni Ukristo wa Kanisa Katoliki. Wakazi Wakristo kwa jumla ni 83.2%.
Wananchi wachache, wageni wengi
haririIdadi ya wakazi ni takriban 35,000 ambao 5,070 au 16% ya wakazi wote ni wananchi na wengine wote ni wageni wanaoishi mjini. 47% ya wakazi ni Wafaransa, 16% Waitalia na wengine 21% ni raia wa mataifa 125 mbalimbali.
Nchi ya matajiri wengi
haririMonako haina kodi ya mapato. Hali hii imesababisha matajiri wengi kutoka nchi mbalimbali kuhamia nchini. Hivyo Monako ni nchi yenye asilimia kubwa ya mamilionea kulingana na idadi ya wakazi wote kuliko nchi yoyote duniani.
Historia
haririHistoria ya Monako imekuwa sawa na historia ya familia ya Grimaldi tangu mwanzo wake.
Akina Grimaldi walikuwa matajiri katika mji wa Genova (Italia) waliopaswa kukimbia nchi wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1296 BK. Walinunua cheo cha kitemi pamoja na maeneo madogomadogo ya utawala katika Italia ya Kaskazini hadi Ufaransa Kusini.
Kati ya maeneo haya yote ni Monako pekee iliyobaki mikononi mwao tangu kuondoa mji mikononi mwa Genova mwaka 1419.
Watemi wa Grimaldi walifaulu kwa siasa yenye busara kupata kibali cha Wafalme wa Ufaransa kuwa eneo la kujitegemea bila mamlaka ya kifalme juu yao. Wakati ule palikuwapo na nchi nyingi ndogo sana za aina hiyo katika Ulaya, hasa Italia na Ujerumani.
Busara ya akina Grimaldi iliwawezesha kutunza uhuru wao katika karne zilizofuata, hasa wakijenga uhusiano mzuri mara na huyu mara na huyu kati ya majirani wakubwa.
Kati ya 1425 hadi 1641 akina Grimaldi waliweka nchi yao chini ya ulinzi wa Hispania wakiwalipa Wahispania pesa kwa kuweka kikosi cha wanajeshi katika boma la Monako. Tendo hilo lilikuwa utetezi dhidi ya wafalme wa Ufaransa ambao wakati mwingine walielekea kumeza nchi ndogo.
Baada ya kuchoka na Wahispania walifanya mapatano na Wafaransa waliolazimisha Hispania kuondoka.
Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789 utawala wa kifalme na kitemi ulifutwa kabisa Ufaransa na serikali ya mapinduzi haikuheshimu tena mapatano ya kukubali uhuru wa eneo la akina Grimaldi.
Lakini baada ya kipindi cha Napoleon Bonaparte, aliyerithi matunda ya mapinduzi, mataifa ya Ulaya kwenye mkutano wa Vienna mwaka 1815 yalipatana kurudisha hali jinsi ilivyowahi kuwa awali. Hivyo Wagrimaldi walirudi Monako wakiendelea kutawala hadi leo.
Nchi lindwa ya Ufaransa
haririTangu 1918 Monako ni nchi lindwa ya Ufaransa yenye uhuru katika mambo ya ndani lakini kwa masharti kuhusu mambo ya nje. Ufaransa ina haki ya kutaja majina kwa ajili ya nafasi za Mkuu wa Polisi na Mwanasheria Mkuu.
Kiuchumi ni sehemu ya Ufaransa isipokuwa ina sheria zake juu ya kodi. Hivyo ni pia sehemu ya eneo la forodha la EU bila kuwa mwanachama wa EU.
Lakini Monako ni mwanachama wa UM na wa Halmashauri ya Ulaya.
Mkataba wa 1918 una kipengele cha kwamba uhuru wa nchi utakwisha kama hakutakuwa na mrithi tena wa familia ya Grimaldi atakayechukua cheo cha mtemi. Mtoto wa kupanga atakubaliwa kama mrithi.
Viungo vya Nje
hariri- Monaco Guide for Monaco
- Monaco travel guide kutoka Wikisafiri
- Official website Ilihifadhiwa 11 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- History of Monaco: Primary documents
- Official website of the Prince's Palace of Monaco
- Official website for Tourism
- Monaco Guide for Monaco
- In the House of Grimaldi Ilihifadhiwa 26 Desemba 2005 kwenye Wayback Machine., a reprint of a 1993 article from the author's personal website
- Monaco Eye: Unofficial Guide for Visitors to Monaco Ilihifadhiwa 22 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- Satellite Map of Monaco with Grand Prix track Ilihifadhiwa 7 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Order of the doctors of Monaco
- European Business article Ilihifadhiwa 13 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
- Monaco photo gallery
- Street map of Monaco Ilihifadhiwa 13 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Monako kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |