Peter King'ori Mwangi (alizaliwa mwaka 1970) ni mhandisi wa umeme, mhasibu na mkurugenzi wa biashara nchini Kenya. Kwasasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni na ofisa Mkuu Mtendaji wa UAP Old Mutual Group, shirikisho la huduma za kifedha, lenye makao yake nchini Kenya, lenye matawi katika nchi sita za Afrika..[1][2]

Alizaliwa katika Kaunti ya Nyeri, Kenya mwaka 1970,[1] na alisoma shule za nchini Kenya kabla ya kwenda chuo kikuu. Alipata Shahada ya Awali ya Sayansi katika uhandisi wa umeme kwenye Chuo Kikuu cha Nairobi, akihitimu mnamo mwaka 1993.[3] Pia ni mhasibu halali wa umma na mchambuzi wa masuala ya fedha. Peter ni mwanachama wa Taasisi ya Makatibu Wakuu wa Kenya (ICPSK).[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 Bloomberg Research (20 Septemba 2017), Executive Profile of Peter King'ori Mwangi, Group CEO & Executive Director, UAP Old Mutual Group, Bloomberg Research, iliwekwa mnamo 20 Septemba 2017{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Nation Reporter (30 Juni 2015). "Former NSE boss Peter Mwangi named CEO of UAP-Old Mutual Group". Daily Nation. Nairobi. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Kiarie, Lillian (5 Agosti 2014). "Why public is being offered a piece of Nairobi Securities Exchange". The Standard (Kenya). Nairobi. Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter Mwangi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.