Kaunti ya Nyeri
- Kuhusu mji, tazama Nyeri
Kaunti ya Nyeri ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Nyeri | |
---|---|
Kaunti | |
Kilele cha Lenana katika Mlima Kenya, Kaunti ya Nyeri | |
Nyeri County in Kenya.svg Kaunti ya Nyeri katika Kenya | |
Nchi | Kenya |
Namba | 19 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati |
Makao Makuu | Nyeri |
Miji mingine | Karatina, Othaya, Kiganjo |
Gavana | Edward Mutahi Kahiga |
Seneta | Ephraim Maina |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Rahab Mukami Wachira |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Nyeri |
Eneo | km2 3 325 (sq mi 1 284) |
Idadi ya watu | 759,164 |
Wiani wa idadi ya watu | 228 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | nyeri.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 759,164 katika eneo la km2 3,325, msongamano ukiwa hivyo wa watu 228 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Nyeri.
Jiografia
haririKaunti ya Nyeri imepakana na Laikipia (kaskazini), Kirinyaga (mashariki), Murang'a (kusini) na Nyandarua (magharibi).
Topografia ya kaunti huwa na miinuko mikali na mabonde. Mlima Kenya hupatikana katika mpaka wa Meru na Nyeri. Mto Chania na Mto Sagana ndiyo mito mikubwa ambayo hupitia katika kaunti hii[2].
Utawala
haririKaunti ya Nyeri imegawanyika ifuatavyo[3]:
Eneo bunge/kaunti ndogo | Kata |
---|---|
Tetu | Dedan Kimathi, Wamagana, Aguthi-Gaaki |
Kieni | Mweiga, Naromoro, Kiamathaga, Mwiyogo/Endarasha, Mugunda, Gatarakwa, Thegu River, Kabaru, Gakwa |
Mathira | Ruguru, Magutu, Iriaini, Konyu, Kirimukuyu, Karatina Town |
Othaya | Mahiga, Iria-ini, Chinga, Karima |
Mukurweini | Gikondi, Rugi, Mukurwe-ini West, Mukurwe-ini Central |
Nyeri Town | Kiganjo/Mathari, Rware, Gatitu/Muruguru, Ruring'u, Kamakwa/Mukaro |
- Tetu 80,453
- Kieni East 110,376
- Kieni West 88,525
- Mathira East 99,065
- Mathira West 59,895
- Nyeri South 91,081
- Mukurwe-ini 89,137
- Nyeri Central 140,338
- Mt. Kenya Forest 188
- Aberdare Forest 106
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ A REVIEW OF NYERI COUNTY-KENYA STRATEGIC PLAN 2013 – 2017, iliwekwa mnamo 29/04/2018
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Nyeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |