Philemon Ndesamburo

Philemon Kiwelu Ndesamburo (alifahamika kama ‘Mzee Ndesamburo’; 19 Februari 1935 - 31 Mei 2017) alikuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.[1] Alipata nafasi ya kuwa mbunge kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mwanasiasa huyo aliingia katika kinyang’anyiro hicho na kufanikiwa kuwa mbunge tangu mwaka 2000.

Philemon Ndesamburo


Mbunge
wa Moshi Mjini
Muda wa Utawala
Novemba 2000 – Novemba 2015
aliyemfuata Jaffary Michael

tarehe ya kuzaliwa (1935-02-19)19 Februari 1935
Tanganyika
tarehe ya kufa 31 Mei 2017 (umri 82)
Moshi, Tanzania
utaifa Mtanzania
chama CHADEMA

Alifariki dunia katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi alikokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa za kifo chake zilithibitishwa na Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Basil Lema. Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo aliongoza ibada ya mazishi ya mwanasiasa mkongwe iliyofanyika katika Kanisa la Lutheran Kiboroloni.

Katika mahubiri kwenye ibada hiyo Askofu Shoo alisema kifo cha Ndesamburo kimeacha pengo kubwa kwa familia na taifa la Tanzania kutokana na mchango wake wa pekee. “Mzee Ndesamaburo alikuwa mzalendo wa Tanzania ambaye hakumbagua mtu yeyote bila kujali dini yake, kabila au chama cha siasa. Zaidi ya yote, Mzee Ndesamburo alikuwa mtu mwenye hofu ya Mungu,” alisema Askofu Shoo Jumatano ya Juni 7, 2017.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. "Mengi kuhusu Philemon Ndesamburo". 17 Julai 2006. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-26. Iliwekwa mnamo 11 Novemba 2011.