Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ni muungano wa Walutheri katika nchi ya Tanzania.
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania | |
---|---|
Mkuu wa kanisa: | Askofu Dk. Alex Malasusa |
Uhusiano: | All Africa Conference of Churches (AACC) Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) World Lutheran Federation |
Idadi ya dayosisi: | 24 |
Wanachama: | Milioni 8 hivi |
Anuani ya barua: | P.O. Box 3033 Arusha, Tanzania |
Tovuti rasmi: | https://elct.or.tz/ |
Mwaka 1938 makanisa saba ya Kilutheri yaliungana kama Muungano wa Makanisa ya Kilutheri, na tarehe 19 Juni 1963 yakawa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.[1]
Lengo la KKKT ni kuwapa watu nafasi ya kumfahamu Yesu Kristo ili kupata uzima wa milele. Kanisa limejengwa juu ya msingi wa Yesu Kristo, linaongozwa na Neno la Mungu kama linavyopatikana katika Agano la Kale na Agano Jipya (Biblia ya Kikristo), na limeimarishwa katika sakramenti.
KKKT linaongozwa na Mkuu wa kanisa (Askofu Mkuu[2]) na maaskofu ishirini na sita kutoka dayosisi ishirini na saba, wakiwa na wanachama zaidi ya milioni 8 hivi [3] wanaolifanya kuwa la pili duniani kati ya makanisa ya Kilutheri (baada ya lile la Uswidi).
Ofisi kuu ya KKKT iko katika mji wa Arusha.
KKKT lina uhusiano na All Africa Conference of Churches (AACC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Lutheran World Federation (LWF) na Lutheran Mission Cooperation (LMC).
KKKT ni chama kinachowapa wanachama chake nafasi ya kumwabudu Mungu, kupata elimu ya Kikristo na huduma nyingi nyingine.
Matawi
- Elimu (Sekondari na Chuo Kikuu)
- Fedha na Utawala
- Afya na Utabibu (Hospitali 21 na zahanati nyingi)
- Umisheni na Uinjilisti
- Upangaji na Maendeleo
- Hudumu ya Jamii na Kazi ya Akinamama
Dayosisi
|
Tanbihi
- ↑ "Homepage". Evangelical Lutheran Church in Tanzania. 2007. Iliwekwa mnamo 2008-12-17.
- ↑ https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/mabadiliko-ya-kishindo-kkkt-4348180
- ↑ "Evangelical Lutheran Church in Tanzania". News and Events. EECMY. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 1, 2016. Iliwekwa mnamo Desemba 1, 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-25. Iliwekwa mnamo 2010-09-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-02. Iliwekwa mnamo 2010-09-12.
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Evangelical Lutheran Church in Tanzania Tovuti rasmi ya KKKT
- (Kiingereza) Lutheran Mission Cooperation Archived 21 Desemba 2008 at the Wayback Machine. Tovuti rasmi ya LMC