Chura-kucha
(Elekezwa kutoka Pipidae)
Chura-kucha | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Chura-kucha wa Afrika (Xenopus laevis)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 5:
|
Vyura-kucha ni aina za vyura ambao wanaishi majini maisha yao yote. Miguu yao ya nyuma ina ngozi katikati ya vidole lakini miguu ya mbele hainayo, isipokuwa vyura-kucha wadogo ambao wana ngozi katikati ya vidole vya miguu yote. Kuna vidole vitano kwa miguu ya nyuma lakini vidole vinne kwa miguu ya mbele. Vidole vitatu vya miguu ya nyuma vina ukucha mweusi. Mwili wao ni mpanapana na ngozi ni ya kuteleza kwa sababu ya ute mwingi. Vyura hawa hawana ulimi. Hufanya sauti kama mialiko kwa mfupa wa hayoidi (hyoid bone).
Spishi za Afrika
hariri- Hymenochirus boettgeri, Chura-kucha Mdogo wa Kongo (Congo dwarf clawed frog)
- Hymenochirus boulengeri, Chura-kucha Mdogo Mashariki (Eastern dwarf clawed frog)
- Hymenochirus curtipes, Chura-kucha Mdogo Magharibi (Western dwarf clawed frog)
- Hymenochirus feae, Chura-kucha Mdogo wa Gaboni (Gaboon dwarf clawed frog)
- Pseudhymenochirus merlini, Chura-kucha Mdogo wa Merlin (Merlin's dwarf grey frog)
- Silurana epitropicalis, Chura-kucha wa Kameruni (Cameroon clawed frog) – inaainishwa katika Xenopus pia
- Silurana tropicalis, Chura-kucha Magharibi (Western clawed frog) – inaainishwa katika Xenopus pia
- Xenopus amieti, Chura-kucha wa Amiet (Volcano clawed frog)
- Xenopus andrei, Chura-kucha wa André (André's clawed frog)
- Xenopus borealis, Chura-kucha Kaskazi (Marsabit clawed frog)
- Xenopus boumbaensis, Chura-kucha wa Mawa (Mawa clawed frog)
- Xenopus clivii, Chura-kucha wa Eritrea (Eritrea clawed frog)
- Xenopus fraseri, Chura-kucha wa Fraser (Fraser's clawed frog)
- Xenopus gilli, Chura-kucha Kusi (Cape clawed toad)
- Xenopus itombwensis, Chura-kucha wa Itombwe (Itombwe Massif clawed frog)
- Xenopus laevis, Chura-kucha wa Afrika (African clawed frog)
- Xenopus largeni, Chura-kucha Habeshi (Largen's clawed frog)
- Xenopus lenduensis, Chura-kucha wa Lendu (Lendu Plateau clawed frog)
- Xenopus longipes, Chura-kucha wa Ziwa Oku (Lake Oku clawed frog)
- Xenopus muelleri, Chura-kucha wa Müller (Müller's clawed frog)
- Xenopus petersii, Chura-kucha wa Peters (Peters's clawed frog)
- Xenopus pygmaeus, Chura-kucha wa Bouchia (Bouchia clawed frog)
- Xenopus ruwenzorensis, Chura-kucha wa Uganda (Uganda clawed frog)
- Xenopus vestitus, Chura-kucha wa Kivu (Kivu clawed frog)
- Xenopus victorianus, Chura-kucha wa Ziwa Viktoria (Lake Victoria clawed frog)
- Xenopus wittei, Chura-kucha wa De Witte (De Witte's clawed frog)
Spishi za Amerika ya Kusini
hariri- Pipa arrabali (Arrabal's Suriname toad)
- Pipa aspera (Albina Surinam toad)
- Pipa carvalhoi (Carvalho's Surinam toad)
- Pipa myersi (Myers's Surinam toad)
- Pipa parva (Sabana Surinam toad)
- Pipa pipa (Common Surinam toad)
- Pipa snethlageae (Utinga Surinam toad)
Picha
hariri-
Chura-kucha mdogo wa Kongo
-
Chura-kucha wa Kameruni
-
Chura-kucha magharibi
-
Chura-kucha wa Amiet
-
Chura-kucha wa Fraser
-
Chura-kucha wa Ziwa Oku
-
Carvalho's Surinam toad
-
Common Surinam toad