Domomwiko

Jenasi ya ndege wakubwa wa maji wenye domo la umbo la mwiko
(Elekezwa kutoka Plateinae)
Domomwiko
Domomwiko wa Afrika
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Pelecaniformes (Ndege kama wari)
Familia: Threskiornithidae (Ndege walio na mnasaba na kwarara)
Nusufamilia: Plataleinae (Ndege wanaofanana na domomwiko)
Jenasi: Platalea
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 6:

Domomwiko ni ndege wa nusufamilia Plataleinae katika familia ya Threskiornithidae ambao wana miguu mirefu na domo lenye umbo wa mwiko. Rangi yao ni nyeupe isipokuwa Roseate Spoonbill ambaye ana rangi ya pinki. Hulipeleka domo lao huku na huku katika maji machache na wakisikia kiumbe mdogo kama samaki mdogo, mdudu au gegereka, hulifunga upesi ili kukamata windo. Hujenga tago lao juu ya miti au matete, mara nyingi pamoja na kwarara, yangeyange na koikoi. Jike huyataga mayai 2-5.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri