Mdudu mabawa-msuko

(Elekezwa kutoka Plecoptera)
Mdudu mabawa-msuko
Mdudu mabawa-msuko (Perla marginata)
Mdudu mabawa-msuko (Perla marginata)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Lang, 1888
Oda: Plecoptera
Burmeister, 1839
Ngazi za chini

Nusuoda 2, familia 16:

Wadudu mabawa-msuko ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Plecoptera (plekein = kusuka, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wadudu hawa huishi majini baridi katika muundo wa nayadi (lava ya wadudu wa maji) kwa muda wa mwaka mmoja hadi miaka minne kufuatana na spishi, halafu hutoka kwenye maji na kuambua na kuwa mdudu aliyekomaa wenye mabawa. Hawa ni wadudu sahili bila viungo vya kiwiliwili vilivyotoholewa. Wana viungo vya kinywa vinavyotumika kwa kutafuna, vipapasio virefu vyenye pingili nyingi, macho makubwa ya kuungwa, oseli tatu (macho ya msingi) na mikia miwili mirefu (kwa kweli serki zilizorefuka). Wasiporuka wanakunja mabawa juu ya fumbatio. Nayadi wanafanana na mdudu mpevu lakini hawana mabawa na wana matamvua. Nayadi wengi zaidi hukamata arithropodi wengine wa maji, lakini nayadi wa spishi nyingine hula maada ya mimea. Wadudu wapevu hula mimea lakini wengine hawali kabisa.

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu mabawa-msuko kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hiyo kuhusu "Mdudu mabawa-msuko" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.