Postikadi (kutoka ing. post card) ni aina ya barua isiyo na bahasha. Kwa kawaida ni kipande cha kistatili cha karatasi ngumu chenye ujumbe mfupi unaotumwa kwa posta.

Postikadi yenye picha ya meli
Upande wa nyuma wenye anwani, stempu ma ujumbe mfupi

Mara nyingi postikadi huwa na picha upande mmoja halafu anwani, stempu na ujumbe mfupi upande wa kinyume. Gharama ya postikadi ni kidogo chini ya gharama ya barua katika bahasha.

Ilhali postikadi haina bahasha ujumbe wake unaweza kusomwa na kila mtu anayeishiska. Kadi hizi zilianza kutumiwa kuanzia miaka ya 1860. Tangu kuwa na bei ndogo kuliko barua idadi ya postikadi kati ya barua iliongezeka. Baada ya kupatikana kwa simu za mkononi, sms na barua pepe postikadi zimepungua sana. Bado zinatumiwa hasa na watu waliosafiri wakitaka kutuma picha ya mahali walipofika.

Kadi za posta za kwanza zilipendekezwa na mkurugenzi wa posta ya Prussia Heinrich von Stefan mnamo 1865, lakini pendekezo lake lilikataliwa kwa sababu mamlaka iliona "umbo lisilofaa kwa kutuma ujumbe"[1] Lakini kwenye mwaka 1869 fomati hiyo ilikubaliwa na posta ya Austria-Hungaria ikafanyikiwa na kuenea.[2]

Tanbihi hariri

  1. Historia ya postikadi.
  2. Tweeting by mail: The postcard’s stormy birth , tovuti ya Los Angeles Times, June 22, 2013

Viungo vya Nje hariri