Nzi-gome

(Elekezwa kutoka Psocoptera)
Nzi-gome
Metylophorus nebulosus
Metylophorus nebulosus
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Psocodea
Hennig, 1966
Ngazi za chini

Nusuoda 3:

Nzi-gome (kutoka Kiing.: barkfly) ni wadudu wadogo (mm 1-10) wa oda Psocodea (psokhos = iliyotafunwa, ptera = mabawa) katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Spishi zinazoishi ndani ya majengo huitwa chawa-vitabu. Zamani spishi fulani za nusuoda Troctomorpha ziligeuka kuwa chawa vidusia. Kwa hivyo siku hizi wataalamu wanaweka chawa katika Psocodea kama oda ndogo Phthiraptera chini ya Troctomorpha.

Wadudu hawa wana mwili kwa muundo wa msingi. Paji ya kichwa imefura, macho ni makubwa kwa kulinganisha na wana oseli tatu. Mandibuli ni kwa kutafuna na ndewe ya kati ya maxila imegeuka katika kifito ambacho kinakaza mdudu akiparua mboji. Wakiwa na mabawa, haya huwekwa kama hema. Pengine urefu wa yale ya mbele ni 50% zaidi ya yale ya nyuyma.

Jenasi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Afrotrogla
  • Amphientomum
  • Amphigerontia
  • Amphipsocus
  • Archipsocus
  • Blaste
  • Blastopsocidus
  • Cerobasis
  • Echmepteryx
  • Ectopsocopsis
  • Ectopsocus
  • Elipsocus
  • Epipsocus
  • Fuelleborniella
  • Ghesquierella
  • Haematomyzus
  • Haplophallus
  • Harpezoneura
  • Hemiseopsis
  • Hemipsocus
  • Heterocaecilius
  • Isophanes
  • Isophanopsis
  • Lachesilla
  • Lepinotus
  • Lesneia
  • Liposcelis
  • Lophopterygella
  • Maoripsocus
  • Mepleres
  • Mesopsocus
  • Nanopsocus
  • Nepticulomima
  • Paracaecilius
  • Pearmania
  • Perientomum
  • Peripsocus
  • Pilipsocus
  • Pseudocaecilius
  • Pseudoseopsis
  • Psocathropos
  • Psocidus
  • Psococerastis
  • Psoculidus
  • Psylloneura
  • Ptycta
  • Rhyopsocus
  • Schizopechus
  • Sigmatoneura
  • Stenocaecilius
  • Stimulopalpus
  • Tarsophilus
  • Thylacella
  • Thylax
  • Trichadenotecnum
  • Trogium
  • Valenzuela
  • Xenopsocus
  • Ypsiloneura
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nzi-gome kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu "Nzi-gome" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili barkfly kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni nzi-gome.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.