Purim (פּוּרִים, Pûrîm, yaani bahati, kutoka neno pur,[1] kuhusiana na Kiakadi pūru) ni sherehe ya kila mwaka ya Wayahudi.

Igizo la Purim.

Inaadhimishwa katika tarehe 14 ya mwezi wa Kiyahudi wa Adar, au tarehe 15 sehemu fulanifulani.

Sikukuu hiyo inafanya ukumbusho wa wokovu wa taifa la Israeli lililokabili maangamizi ya kimbari ya halaiki katika dola la Uajemi.

Kadiri ya Kitabu cha Esta, njama hiyo ilishindikana hasa kwa juhudi wa huyo Esta aliyebahatika kuwa malkia wa dola hilo wakati huo.

Tanbihi hariri

  1. Est 9:24, 27.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: