Kuhusu kete ya sataranji tazama: Malkia

Malkia Zauditu wa Ethiopia.

Malkia ni mtawala wa kike juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka kwa mzazi wake aliyekuwa mfalme au malkia pia.

Lakini kuna pia malkia waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingin,e hasa kama mtawala aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Mara nyingi malkia alipatikana kwa njia ya ndoa halafu alishika utawala kama mumewe mfalme mwenyewe alikufa au kugonjeka.

Kukubaliwa au kutokubaliwa kwa mtawala wa kike hariri

Katika historia kuna tofauti kubwa kama nchi iliweza kukubali kutawaliwa na mwanamke. Nchi mbalimbali zilibadilisha sheria zao walipoona ya kwamba mfalme alikosa watoto wa kiume ilhali viongozi waliogopa matatizo ya uchaguzi wa mfalme kutoka familia nyingine.

Mfano wa tofauti hizo ni maungano ya kifalme ya Uingereza na Hannover kati ya 1714 na 1837. Mtemi Georg Ludwig wa Hannover alirithi cheo cha mfalme wa Uingereza na watoto wa kiume wa familia waliendelea kuwa wakuu wa nchi zote mbili. Baada ya kifo cha mfalme William IV, Uingereza ulimteua mpwa wake Viktoria kuwa malkia mpya. Lakini sheria za Hannover hazikukubali mwanamke kama mtawala, hivyo maungano ya kifalme kati ya nchi hizo mbili yalikwisha.

Katika jamii mbalimbali za Afrika mtawala wa kike alikubaliwa tu. Mifano mashuhuri wa malkia wa Kiafrika ni "Negiste Negest" Zauditu wa Uhabeshi (alitawala 1916-1930) au Farao wa kike katika historia ya Misri.

Malkia ya heshima hariri

Kuna pia matumizi ya kiheshima ya neno malkia kwa kumtaja mke wa mfalme hata asiposhika madaraka ya kiutawala.

Tazama pia: hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malkia kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.