Rachid Baba Ahmed

mtayarishaji na mwimbaji wa muziki wa Algeria; mwanamuziki wa raï

Rachid Baba Ahmed (20 Agosti 194615 Februari, 1995) alikuwa mtayarishaji, mtunzi na mwimbaji wa nchini Algeria alijulikana zaidi katika aina ya kikanda inayojulikana kama raï . [1] Alipewa sifa ya umaarufu wa kimataifa wa aina hiyo mnamo mwaka 1976, kupitia wimbo wake wa pop raï.

Kazi hariri

Rachid Baba alitayarisha albamu iliyoitwa Rai Rebels iliyotolewa nchini Marekani. Baba aliwasaidia wasanii wengi wachanga na walio kuwa wanaanza, wakiwemo kama Chaba Fadela na Cheb Sahraoui .

Kifo hariri

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Algeria, aliuawa na wafuasi wa imani kali ya Kiislamu mnamo tarehe 15 Februari, mwaka 1995, nje ya duka lake la kumbukumbu huko Oran, Algeria . [2] Alikuwa mlengwa wa muda mrefu wa harakati za Kiislamu kwa sababu ya kujihusisha kwake katika utayarishaji wa nyimbo zenye mada za mapenzi na maisha ya kila siku. [2]

Marejeo hariri

  1. Al-Taee, Nasser (Spring 2003). "Running with the Rebels: Politics, Identity, and Sexual Narrative in Algerian Rai". Echo 5 (1). Archived from the original on 2018-09-15. Retrieved 2014-10-18. 
  2. 2.0 2.1 "Producer of Rai Music Killed in Algeria". Billboard (Nielsen Business Media) 107 (9): 48. 4 March 1995. ISSN 0006-2510. 
  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rachid Baba Ahmed kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.