Reni
Reni (kutoka jina la Kilatini "Rhenus" la mto Rhine) ni metali nzito na haba sana. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Re na namba atomia 75 katika mfumo radidia.
Reni (Rhenium) | |
---|---|
Reni katika testitubu
| |
Jina la Elementi | Reni (Rhenium) |
Alama | Re |
Namba atomia | 75 |
Mfululizo safu | Metali ya mpito |
Uzani atomia | 98 |
Valensi | 2, 8, 18, 32, 13, 2 |
Densiti | 21.02 |
Ugumu (Mohs) | {{{ugumu}}} |
Kiwango cha kuyeyuka | 3459 K (3186 °C) |
Kiwango cha kuchemka | 5869 K (5596 °C) |
Asilimia za ganda la dunia | 1 · 10-7 % |
Hali maada | mango |
Mengineyo |
Tabia
haririReni ni metali ngumu na nzito. Hutokea katika mitapo ya molibdeni. Baada ya kuisafisha rangi yake ni kifedha-nyeupe. Kati ya elementi zote zisizo nururifu ni elementi haba sana.
Matumizi
haririKutokana na uhaba hakuna matumizi mengi. Inachanganywa hasa ndani ya aloi mbalimbali hasa na nikeli inapoongeza uimara kwa mfano ndani ya injini za ndege.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Reni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |