Richard Vincent Corleleus Petrus (amezaliwa Dar es Salaam, 10 Agosti 1984) ni Mtanzania aliyeshinda katika Big Brother Afrika kwa mwaka wa 2007.

Wasifu

hariri

Maisha ya awali

hariri

Richard ni mtoto wa nne wa familia ya Vincent na Mtanzania Mariam Muhammed ambaye ni Mzaramo.

Babu yake, Richard Corleleus Petrus, alitokea Uholanzi na kuhamia Tsavo National Park nchini Kenya mnamo mwaka 1930, akiwa amejishughulisha katika kuua simba waliokuwa wakiwamaliza watu waliokuwa wakijenga reli ya Mombasa na baadaye alihamia nchini Uganda akitafuta maisha.

Mwaka 1968 Vincent, ambaye alizaliwa Uganda na Richard na binti mfalme wa Rwanda, Mutara Rudahigwa, alimuoa mwanamke wa Kitanzania, Bi. Mariam aliyekuwa akisoma nchini Uganda.

Mwaka 1969 familia ya Vincent ilipata mtoto wa kike aitwaye Brenda aliyefuatiwa na Linda aliyezaliwa mwaka 1972 ambao wote walizaliwa Tanzania pamoja na kuwa wazazi wao walikuwa wakiishi Uganda.

Kuhamia rasmi Tanzania

hariri

Wakati utawala wa Iddi Amin alipopindua utawala wa Milton Obote mnamo mwaka wa 1972, na sera yake ya kunyang’anya mali na kulazimika kuwekwa kizuizini mji wa Nakuru, Vicent alishawishiwa na mkewe kuhamia Tanzania na familia hiyo ilihamia Tanzania mwaka 1976 na kuishi Ilala na baadaye kuhamia Makumbusho ambako ndiko alipata watoto wake Edward, Richard na Louis.

Elimu ya Richard

hariri

Richard alianza elimu ya msingi katika shule ya Makumbusho mnamo mwaka 1990 ambako alisoma mpaka mwaka 1993 na mwaka 1994 alihamia katika shule ya msingi Mashujaa ambako hakumaliza mwaka na mwaka 1995 alijiunga na shule ya msingi ya Vincent Alex, iliyopo mjini Kampala, Uganda.

Mwaka 1998 Richard alijiunga na shule ya sekondari ya Makerere iliyopo karibu na Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, ambako alisoma kwa miaka miwili na mwaka 2000 alihamia shule ya Jinja ambako alihitimu elimu yake ya kidato cha nne.

Mwaka 2002 alijiunga na kidato cha tano katika shule ya Makerere na mwaka 2003 alirejea nchini Tanzania baada ya kumaliza masomo yake.

Viungo vya Nje

hariri