Robert Bunsen
Robert Wilhelm Eberhard Bunsen (matamshi ya Kiingereza / bʌnsən /; ila ya Kijerumani: [bʊnzən]; 30 Machi[1] 1811 - 16 Agosti 1899) alikuwa mwanakemia wa Ujerumani.
Alifanya uchunguzi wa vipimo vya moto, na aligundua cesium (mwaka 1860) na rubidium (mwaka wa 1861) na mwanafizikia Gustav Kirchhoff.
Bunsen aliendeleza mbinu nyingi za uchambuzi wa gesi, na alifanya kazi mapema katika uwanja wa kemia ya organoarsenic.
Pamoja na msaidizi wake wa maabara, Peter Desaga, alianzisha kifaa cha Bunsen Burner.
Maisha
haririRobert Bunsen alizaliwa huko Göttingen mwaka 1811.
Baada ya kuhudhuria shule huko Holzminden, Bunsen aliondoka Göttingen mwaka 1828 na alifundishwa kemia na Friedrich Stromeyer pamoja na mineralojia na Johann Friedrich Ludwig Hausmann na alifundishwa hisabati na Carl Friedrich Gauss.
Tanbihi
hariri- ↑ Bunsen mwenyewe aliadhimisha siku ya kuzaliwa kwake siku ya 31 katika miaka yake ya baadaye. Lockemann hata hivyo aliona tarehe 30 kama tarehe sahihi.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Robert Bunsen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |