Robert Mangaliso Sobukwe
Robert Mangaliso Sobukwe (1924-1978) alikuwa mwanasheria na mwanasiasa wa Afrika Kusini aliyeanzisha Pan Africanist Congress kupinga ubaguzi wa rangi nchini. Kwa ajili hiyo alifungwa kwa muda mrefu. Alikuwa muasisi wa chama hicho kilichopigania uhuru wa Waafrika kikijitenga kutoka kwa African National Congress, pia anahusishwa na kuandaa maandamano ya kihistoria ya Shapeville mnamo 1960 yaliyopinga sheria ya Weusi kutembea na vitambulisho ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa kisha Sobukwe kuswekwa jela kunako visiwa vya Rubeni kwa miaka tisa.
Sobukwe alifariki mwaka 1978 kwa saratani na mapafu licha ya wengine kudai kuwa alipewa sumu akiwa jela.
Maisha ya awali
haririSobukwe alizaliwa katika eneo la Graaff-Reinet katika jimbo la Cape Town tarehe 5 Desemba 1924.[1] akiwa mtoto wa mwisho katika familia ya kimaskini ya watoto sita.
Alisoma katika chuo cha Methodist na baadae chuo kikuu cha Fort Hare University akiwa huko ndipo alipojiunga na chama cha African National Congress na mwaka 1948 alichaguliwa kuwa rais wa baraza la wanafunzi .[2]: 420
Marejeo
hariri- ↑ "Robert Mangaliso Sobukwe", South African History Online.
- ↑ Maaba, Brown Bavusile (2001). "The Archives of the Pan Africanist Congress and the Black Consciousness-Orientated Movements". History in Africa. 28: 417–438. doi:10.2307/3172227. JSTOR 3172227.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Robert Mangaliso Sobukwe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |