Rosa Mistika ni kitabu cha kwanza cha riwaya kilichoandikwa na Euphrase Kezilahabi mwaka 1971. Kinahusu wanafunzi wa kike walionyanyaswa na walimu wao[1][2][3].

Matokeo

hariri

Kitabu hicho kiliwahi kusambaa sana lakini baadaye kilikumbwa na rungu la udhibiti kutokana na kuandika uongozi wa hovyo wa tabaka tawala la viongozi wa serikali, wanaotumia nguvu ya siasa na mali za umma kujinufaisha wenyewe, huku wakinyanyasa, kukandamiza na kunyonya tabaka la wanyonge.

Kitabu hiki kilipigwa marufuku kwa sababu zisizo na ukweli wowote, kwa mfano katika ukurasa wa 10, kupitia mhusika Rosa, wanawake wengi walidai kuwa wamedhalilishwa.

Hata hivyo viongozi wa dini pia walidai wamedhalilishwa kupitia jina la Rosa Mistica, lenye maana ya Bikira Maria, na kusema kuwa neno hilo limetumika kwa maana mbaya ya Rosa kama mwanamke malaya, mzinzi na mchafu.

Hivyo basi, kitabu hiki kilizuiliwa kufundishia shuleni na kupigwa marufuku, japokuwa ukweli wa kitabu hiki ni kufichua na kulisema tabaka la viongozi wa juu, jambo ambalo halikuwapendeza viongozi hao.

Hatimaye kilianza kutumika katika shule za sekondari za Tanzania na Kenya[4].

Tanbihi

hariri
  Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rosa Mistika kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.