Rukuba ya Rami


Rukuba ya Rami (lat. & ing. Rukbat, pia α Alfa Sagittarii, kifupi Alfa Sgr, α Sgr) ni kati ya nyota angavu kwenye kundinyota la Kausi (Mshale) (Sagittarius).

Rukuba ya Rami (Alfa Sagittarii, Rukbat)
Rukuba ya Rami (Rukbat) katika kundinyota lake la Kausi (Sagittarius)
Kundinyota Kausi (Mshale) (Sagittarius)
Mwangaza unaonekana 3.97[1]
Kundi la spektra B8 V
Paralaksi (mas) 30.49
Umbali (miakanuru) 182
Mwangaza halisi +0.23
Masi M☉ 2.95
Nusukipenyo R☉ 2.49
Mng’aro L☉ 117
Jotoridi usoni wa nyota (K) 12387
Majina mbadala CD−40° 13245, FK5 728, GC 26737, HD 181869, HIP 95347, HR 7348, SAO 325060, PPM 353699

JinaEdit

Nyota ya Rukuba ya Rami inayomaanisha “goti la mpiga mishale” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. [2]. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaoijua kama ركبة الرامي rukba ar-rami wakitafsiri maelezo katika Almagesti “kwenye goti la mguu wa kushoto”. [3].

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota hii kwa tahajia ya "Rukbat" [4].

Alfa Sagittarii ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu ya 16 katika Kausi ingawa Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki. Hii ni mfano jinsi gani Bayer hakufuata mwangaza kikamilifu wakati wa kugawa majina ndani ya kundinyota.

TabiaEdit

Rukuba ya Rami ni nyota yenye rangi ya buluu maana ina jotoridi kubwa. Nyuzi za Kelvini 12300 zinaendana pamoja na mng’aro wake ulio zaidi ya mara 100 wa ule wa Jua letu ingawa masi yake ni mara tatu ya Jua tu.

Utafiti wa spektra yake unaonyesha ya kwamba nyota hii inazungukwa na wingu la vumbi na mara nyingi mawingu ya aina hii ni asili ya sayari ingawa hadi sasa hakuna sayari iliyotambuliwa. Spektra inaonyesha vilevile dalili za kuwa na nyota msindikizaji lakini pia hii haikuthibitishwa bado.

TanbihiEdit

  1. Vipimo kufuatana na Docobo et al. (2007)
  2. ling. Knappert 1993
  3. Allen, Star-Names (1899), uk. 357, Tooner, Almagest ,uk. 374
  4. Naming Stars, tovuti ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017

Viungo vya NjeEdit


MarejeoEdit

  • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 (online kwenye archive.org)
  • David, Trevor J.; Hillenbrand, Lynne A. (2015), "The Ages of Early-Type Stars: Strömgren Photometric Methods Calibrated, Validated, Tested, and Applied to Hosts and Prospective Hosts of Directly Imaged Exoplanets", The Astrophysical Journal, 804 (2): 146 online hapa
  • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
  • Ptolemy's Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano