Alfa
Alfa (kwa Kiingereza: alpha) ni herufi ya kwanza ya Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa Α (herufi kubwa ya mwanzo) au α (herufi ndogo ya kawaida).
Alfabeti ya Kigiriki | |||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|
Herufi za kawaida | |||||||
Α α Alfa | 1 | Ν ν Ni | 50 | ||||
Β β Beta | 2 | Ξ ξ Ksi | 60 | ||||
Γ γ Gamma | 3 | Ο ο Omikron | 70 | ||||
Δ δ Delta | 4 | Π π Pi | 80 | ||||
Ε ε Epsilon | 5 | Ρ ρ Rho | 100 | ||||
Ζ ζ Dzeta | 7 | Σ σ ς Sigma | 200 | ||||
Η η Eta | 8 | Τ τ Tau | 300 | ||||
Θ θ Theta | 9 | Υ υ Ipsilon | 400 | ||||
Ι ι Iota | 10 | Φ φ Phi | 500 | ||||
Κ κ Kappa | 20 | Χ χ Khi | 600 | ||||
Λλ Lambda | 30 | Ψ ψ Psi | 700 | ||||
Μ μ Mi | 40 | Ω ω Omega | 800 | ||||
Herufi za kihistoria1 | |||||||
Digamma | 6 | San | 90 | ||||
Stigma | 6 | Sho | 90 | ||||
Heta | 8 | Koppa | 90 | ||||
Sampi | 900 | ||||||
1 Viungo vya Nje: Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje |
Katika Ugiriki ya Kale ilihesabiwa pia kama namba "1".
Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za Kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na fisikia. Kundinyota hili limejulikana hasa kama jina la pembe ya kwanza katika pembetatu.
Katika astronomia inatumiwa kuanza hesabu ya nyota katika kundinyota. Kwa mfano nyota yetu jirani katika ulimwengu inaitwa "Alfa Centauri". Imeitwa hivyo kwa sababu inang'aa kushinda nyota zote za kundinyota ya Centaurus. Inayofuata ni "beta Centauri" na kadhalika.
Alfa ikiwa herufi ya kwanza ya alfabeti ya Kigiriki hutumiwa pia kwa kutaja mwanzo. Hivyo ni kinyume cha mwisho au omega. Usemi wa Biblia ya Kikristo hujulikana kuhusu Mungu kuwa ni "Alfa na Omega, mwanzo na mwisho" (Ufunuo wa Yohane 21:6).