Rustiko wa Narbonne
Rustiko wa Narbonne (alifariki Narbonne, Ufaransa, 461 hivi) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 427 au 430. Alifanya hivyo ingawa alipenda zaidi maisha ya ndani ya monasteri.
Kama askofu alishiriki Mtaguso wa Efeso (431)[1].
Baada ya mji huo kutekwa na Wagothi waliomtawaza askofu wa madhehebu yao ya Kiario, alimuandikia Papa Leo I barua ya kujiuzulu, lakini Papa alimhimiza asiache[2]. Hapo alijitahidi kuimarisha Wakatoliki.
Mwaka 451, pamoja na wenzake 43, aliunga mkono barua ya Papa Leo I kwa Flaviano wa Kostantinopoli dhidi ya wafuasi wa Nestori.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Tazama pia Edit
Tanbihi Edit
- ↑ Benedictines, Encyclopedia.
- ↑ Epistle CLXVII.
- ↑ Martyrologium Romanum
Vyanzo Edit
- Ekkart Sauser, Rusticus: hl. Bischof von Narbonne, 1262
Marejeo mengine Edit
- Marrou, Henri-Irenee, "Le dossier epigraphique de l'eveque Rusticus de Narbonne," Rivista di archeologia cristiana 3-4 (1970) pp 331– 349.
Viungo vya nje Edit
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |