SEO (kifupi cha maneno ya Kiingereza: search engine optimization) ni utaratibu wa kuongeza ubora na wingi wa watembeleaji wa tovuti kwa kuongeza upatikanaji wa tovuti au ukurasa mmojawapo wa tovuti kwa watumiaji wa tovuti za kutafuta kurasa na habari mtandaoni.[1]
Utaratibu huo unajumuisha tu uboreshaji usiotumia malipo ya matangazo.

SEO inaweza kulenga tovuti za kutafuta za aina mbalimbali kama vile utafutaji wa picha, utafutaji wa video, majarida ya kitaaluma, [2] utafutaji wa habari na utafutaji wa kisekta.

Uboreshaji wa tovuti unaweza kujumuisha kuhariri habari zilizomo kwenye tovuti hiyo, kuboresha HTML na mbinu nyingine nyingi. Baadhi ya mbinu zinakubalika na tovuti za kutafuta ile mbinu nyingine huonekana kuwa ni za ulaghai.[3]

Kufikia Mei 2015, utafutaji kwa kutumia simu za mkononi ulipiku ule wa kutumia kompyuta.[4]

Kama mbinu ya kujitangaza mtandaoni, https://ozguraltun.com.tr/ Archived 12 Julai 2013 at the Wayback Machine. inatazama jinsi tovuti za kutafuta zinavyofanya kazi, algorithm zinazoonyesha tabia za tovuti za kutafuta, maneno yanatotumiwa na watafutaji, n.k.

Historia

Waangalizi wa tovuti na watoa habari walianza kuboresha tovuti kwa njia hiyo toka katikati ya 1990. Mwanzoni, waangalizi wa tovuti walitakiwa kutuma anwani za tovuti zao kwa tovuti za kutafuta.[5]

Marejeo

  1. "SEO - search engine optimization". Webopedia. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)
  2. Beel, Jöran and Gipp, Bela and Wilde, Erik (2010). "Academic Search Engine Optimization (ASEO): Optimizing Scholarly Literature for Google Scholar and Co" (PDF). Journal of Scholarly Publishing. ku. 176–190. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2017-11-18. Iliwekwa mnamo Aprili 18, 2010. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. "What is Blackhat SEO?" June 14, 2019.
  4. "Inside AdWords: Building for the next moment" Google Inside Adwords May 15, 2015.
  5. Brian Pinkerton. "Finding What People Want: Experiences with the WebCrawler" (PDF). The Second International WWW Conference Chicago, USA, October 17–20, 1994. Iliwekwa mnamo Mei 7, 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje


  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.