Sachsen-Weimar
Sachsen-Weimar (Saksonia-Weimar) ilikuwa moja kati ya maeneo ya watemi wadogo wa Ujerumani ndani ya Dola Takatifu la Kiroma. Ilikuwepo ndani ya eneo la Thuringia ya leo.
Utemi huu ulitokana na kugawiwa kwa urithi wa mtemi Ernest wa Saksonia mwaka 1572. Mji mkuu ulikuwa Weimar.
Ilikuwa nchi ya kujitegemea ndani ya maungano ya Dola Takatifu la Kiroma.
Sachsen-Weimar ilipata umaarufu katika karne ya 18 ambako watawala wake walikusanya washairi na wataalamu katika utemi wao kwa kuwapa heshima na nafasi nzuri za kufanya kazi. Kwa njia hiyo Weimar na chuo kikuu cha utemi mjini Jena zilikuwa kitovu cha utamaduni wa Kijerumani na matengenezo yake.
Washairi wakubwa wa lugha ya Kijerumani kama Goethe na Schiller waliishi Weimar.