Johann Wolfgang von Goethe
Johann Wolfgang von Goethe alikuwa mwandishi, mshairi, mwanasiasa, mwanafalsafa na mwanasayansi Mjerumani anayekumbukwa kama mwandishi mkuu katika fasihi ya Ujerumani.
Alizaliwa mjini Frankfurt am Main tar. 28 Agosti 1749 akafa Weimar 22 Machi 1832. Alisoma sheria lakini alianza kuandika riwaya za kwanza akiwa mwanafunzi.
Waziri mjini Weimar
hariri1775 alipewa kazi ya mshauri wa mtemi wa Sachsen-Weimar na mwaka uliofuata alikuwa waziri katika serikali ya mtemi. Katika miaka ya utumishi wake alishughulika idara nyingi tofauti kama jeshi, fedha, ujenzi wa barabara na elimu. Wakati wake mji mdogo wa Weimar ilipata sifa kubwa ikatembelewa na wageni kutoka Ulaya wote waliotaka kumwona Goethe na Weimar ilikuwa kama kitovu cha utamaduni cha Ujerumani.
Aliendelea kuandika mengi kama riwaya, tamthiliya na mashairi. Tamthiliya ya "Faust" imekuwa kazi yake kuu.
Kazi za kisayansi
haririPamoja na kuandika alianza kujishughulisha na sayansi. Alipenda sana sayansi mpya za biolojia na kemia. Kama waziri alianzisha idara ya kwanza ya kemia ya Ulaya kwenye chuo kikuu cha Jena.
Alifanya utafiti kwenye mifupa ya kiunzi cha mwili akatambua mfupa mmoja kichwani kisichojulikana bado. Aliandika pia kuhusu maumbo ya mimea akajenga misingi ya uainishaji wa kisayansi.
Katika fizikia alitunga nadharia juu ya rangi inayoendelea kujadiliwa kati ya wataalamu hadi leo.
Viungo vya Nje
hariri- Mfano wa shairi ya Goethe kwa Kijerumani na Kiingereza Ilihifadhiwa 7 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.