Salim Ahmedy

mwigizaji, mwongozaji, mwandishi na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania

Salim Ahmedy Issa (amezaliwa Muheza, Tanga, 6 Juni 1983) ni mwigizaji, mwongozaji, mwandishi na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania.[1] Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Gabo Zigamba. Salim amekuwa akisifika kwa umahiri wake katika kuzishika nyusika tofauti. Anafahamika zaidi kwa kucheza filamu ya Big Surprise, Danija, Siyabonga, na nyingine nyingi. Pia ameonekana katika mifululizo ya runinga maarufu kama vile Jua Kali, Kapuni na Baba Olivia.

Salim Ahmed

Gabo—2018
Amezaliwa Salim Ahmed Issa
(1983-06-06)Juni 6, 1983 Muheza, Tanga, Tanzania
Muheza
Jina lingine Gabo Zigamba
Kazi yake Mwigizaji, mwigizaji wa sauti, mtunzi wa filamu, mwongozaji, mtayarishaji
Miaka ya kazi 2008-
Ndoa Latifa Babla Ivan (Tiffany Stores) (2020)
Watoto 4

Maisha ya awali

hariri

Salim alianza elimu ya msingi mnamo 1992 hadi 1998 katika shule ya Iringa Wilolesi. Baadaye sekondari katika shule ya Al-Haramain. Akamaliza 2002. Kuanzia 2003-2006 alijiunga na Chuo Darul Ulumi, Elimu ya Thanawiy. 2006 Chuo Cha Tasuba, Kozi ya Mwaka Mmoja upande wa sanaa. 2007 alijiunga na kampuni ya Super Loaf. Ambapo alifanyakazi mwaka mmoja pekee. Hapo alijikita zaidi kama mhasibu na baadaye akawa mchanganya viambata vya bidhaa.

Mwigizaji, umarufu

hariri

Akiwa katika mahojiano ya kipindi cha Salama Na kinachotupwa mkondoni huko YouTube chini ya Salama Jabir , Salim alitoa siri ya chimbuko la jina la Gabo, "Asili ya jina ni Gabo ni Gabon. Lina maana ya 'sauti isiyosikika" na Zigamba, ni ng'ombe wa kimila aliyekuwa akiabudiwa na Wasukuma zama za kale. Kimsingi, Salim alianza uigizaji rasmi mnamo mwaka wa 2006. Akiwa katika kipindi cha awali kabisa kupoteana na ujalunga, yaani, umri wa miaka 23. Wakati huo alikuwa akisoma Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA). Kabla ya kufika kilele cha kufahamika, alijitupa katika makundi kadhaa ya uigizaji yaliyokuwa jijini Dar es Salaam huku ari ya kutaka kuwa mwigizaji nyota ikifika pomoni. Katika kutimiza ile ndoto ya miaka mingi, hatimaye akawemo katika filamu ya "Olopong" iliyotayarishwa na Al Riyamy Production iliyoongozwa na Khalfan Abdalah, ikafuatiwa na 007 Days.

Atafutaye hachoki, hata akichoka, basi keshapata. Dumu la kutojulikana lilipasuka rasmi mnamo mwaka 2012 baada ya kucheza katika filamu ya "Bado Natafuta." Yaliyomo ndani yake yakaonekana vema. Filamu hiyo alicheza na Patcho Mwamba, Zuberi Mohamed na Shamsa Ford.

Baada ya kufanya kazi, hatmaye akaanzisha kampuni yake ya utayarishaji wa filamu. Akaipa jina la Gabz Media Production (T) Limited.

Filmografia

hariri

Filamu

hariri

Baadhi ya filamu za Gabo;

Filamu za Salim Ahmedy
Na. Jina la filamu Mwaka Uhusika Maelezo
1 Bado Natafuta 2012 Mr. James Mwongozaji Sulesh Marwa, Mtayarishaji Jerumasalem Films
2 Jicho Langu 2014 James Mwongozaji: Leah Mwendamseke

Mtayarishaji: J-Film For Life Production

3 Kona 2015 Mjomba wa Zazuba Mwongozaji: Salim Ahmedy[2]

Utayarishaji: Landline Production

4 Big Surprise 2014 Gabo Mwongozaji: Leah Mwendamseke

Mtayarishaji: J-Film for Life Production

5 Danija 2014 Johnson Mwongozaji: Jacob Steven (JB)

Mtayarishaji: Jerusalem Film Company

6 Safari ya Gwalu 2015 Gwalu Mwongozaji: Daniel Manege

Mtayarishaji: Manege Entertainment

7 Kasanga Nae Mwana 2016 Zigamba Utayarishaji: King Media
8 Heaven Sent 2017 Gabo Mwongozaji: Neema Ndepanya

Mtayarishaji: Endless Fame Production

9 Siyabonga 2017 Siyabonga Mwongozaji: Salum Majagi

Mtayarishaji: Sarafu Media

10 Dr. Okosovo 2018 Dr. Okosovo Kalababash Mwongozaji : Salim Ahmedy

Mtayarishaji: Above The Rim Production

11 Sumu 2018 Salim Mwongozaji: Patrick Komba

Mwongozaji Msaidizi: Salim Ahmedy Mtayarishaji: Third Eye Africa

12 Segere 2019 Chief Segere Mwongozaji: Takura Maurai.

Mtayarishaji: Sarafu Media

13 Kesho 2020 Matete Mkandara Mwongozaji: Salum Majagi

Mtayarishaji : Yusuph Mlela

14 Kigoma 2020 Gabo Mtayarishaji: Mpakasi Films Company
15 Tug of War 2021 Koplo Matata Mwongozaji: Amil Shivji

Mtayarishaji: Kijiweni Film Production

Mifululizo ya Runinga

hariri
Mifululizo ya TV
Na Jina la filamu Mwaka Jina la uhusika Maelezo
1 Kapuni 2019 Mr. Brown DSTV
2 Baba Olivia 2020 Baba Olivia Pendwa App
3 Jua Kali -2023 Diba DSTV
4 Bondeni 2015 ? TBC1 pia ni mtayarishaji
5 Family Love 2017 ? Clouds TV. Pia ni mtayarishaji
6 Maskani 2021 ? Gabz Media

Tuzo na Teuzi

hariri
Mwaka Tamasha Tuzo Mshindi Matokeo
2016 Tuzo za ZIFF Mwigizaji Bora Salim Ahmedy Ameshinda[3]
2017 Tuzo za EATV Mwigizaji Bora ? Ameshinda[4]
Tuzo za ZIFF Mwigizaji Bora ? Ameshinda[5]
2018 Tuzo za EATV[6] Mwigizaji Bora Ameshinda[7]
2018 Tuzo za SIZIFF Mwigizaji Bora Ameshinda[8]
2021 Tanzania Film Festival Mswada Bora wa Filamu Ameshinda[9]

Marejeo

hariri
  1. "Exclusive interview na Gabo; Je ni teja,mmakonde au mchaga?". Bongo Publisher. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-22. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
  2. "Full Interview: Gabo Zigamba Akizungumzia Filamu Yake ya Kona 3". Artists News in Tanzania. 2016-02-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-22. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
  3. Ziff Awards 2016
  4. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named eatv awards
  5. ZIFF Awards 2018
  6. "WAMBURA BABU BLOG: Ridhiwani afunguka ushindi wa Gabo EATV AWARDS". WAMBURA BABU BLOG. 2016-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
  7. Tuzo za EATV
  8. SIZIFF 2018
  9. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named TZFF 2021

Viungo vya Nje

hariri