Sanamu ya Uhuru
Sanamu ya Uhuru (Kiing.:Statue of Liberty) ni sanamu kubwa inayosimama katika bandari ya jiji la New York. Ilifika Marekani mwaka 1885 kutoka Ulaya kama zawadi ya watu wa Ufaransa kwa watu wa Marekani ikasimamishwa na kuzimikwa rasmi 1886..
Sanamu lina kimo cha mita 46.5 na pamoja na msingi wake linafikia mita 93. Inasimama kwenye kisiwa kidogo kilichopo mdomoni mwa bandari.
Imetengenezwa kwa kutumia mabati ya shaba yanayolala juu ya kiunzi cha feleji ndani yake. Kwa jumla uzito wake ni tani 225. Rangi imekuwa kibichi kwa sababu shaba imeoksidishwa kwa nje.
Umbo la sanamu ni mwanamke anayeshika mwenge juu ya kichwa chake. Mwanamke ni ishara ya uhuru na mchongaji alitaka kuweka kumbukumbu ya kufutwa kwa utumwa katika Marekani mwaka 1861. Umbo linaiga mifano ya sanaa ya Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale; mungu wa Kigiriki Helios alionyeshwa kwa mavazi yaleyale na pia na taji kama sanamu ya uhuru; kwa Helios ncha za taji zilikuwa ishara ya mishale ya jua; kwenye sanamu ya uhuru mishale saba inadokeza kwa bahari saba na mabara saba na ujumbe wa uhuru kwa wote. Mwenge ni ishara ya mwangaza unaotoka kwenye uhuru kwa mataifa yote.
Kusudi la zawadi ilikuwa kuweka kumbukumbu kwa uhusiano mwema kati ya Marekani na Ufaransa na msaada uliofika Marekani kutoka Ufaransa wakati wa vita ya uhuru dhidi ya Uingereza.
Baadaye wahamiaji mamilioni waliofika Marekani kwa njia ya meli walisalimiwa na sanamu ya uhuru wakati wa kuingia bandarini.
Sanamu ni kati ya majengo ya Marekani yanayojulikana zaidi.
Viungo vya nje
hariri- (Kiingereza) Tovuti rasmi
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sanamu ya Uhuru kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sanamu ya Uhuru kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |