Sancho Gracia (Madrid, 27 Septemba 1936 - Madrid, 8 Agosti 2012) ni mwigizaji wa filamu wa kawaida na wa katika telesheni, kutoka nchini Hispania.

Sancho Gracia
Sancho Gracia
Sancho Gracia
Jina la kuzaliwa Sancho Gracia
Alizaliwa 27 Septemba 1936, Madrid
Hispania
Kafariki 8 Agosti 2012
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1963 mpaka kifoo.

Sancho pia aliwahi kucheza katika filamu za western ya Italia, maarufu kama Spaghetti western.

Maisha ya Uigizaji hariri

Sancho ameanza shughuli zake za uigizaji kwenye miaka ya 1963, aliweza kushiriki katika filamu moja hivi iitwayo L'Autre femme akiwa pamoja na mwanamama Annie Girardot.

Tangu hapo akaanza kuonekana tena katika filamu nyingine nyingi tu zaidi ya themanini zikiwemo zingine zilifanyiwa huko Hollywoood, mnamo miaka ya 1970 na 1999. Sancho pia aliwahi kushiriki katika filamu moja iitwayo Outlaw Justice humo alishirikiana na Willie Nelson na Kris Kristofferson.

Vile vile, Gracia aliwahi kufanya kazi nchini Australia, alicheza kama mwigizaji wa kawaida katika mfululizo wa televisheni, iliyokuwa inajulikana kama Runaway Island, ya mwaka 1982 na mwaka 1991 akashiriki tena katika filamu ya TV, iliyojulikana kwa jina Pirates Island. Sancho pia pia alishiriki katika tuzo za Oscars na akauteuliwa kuwa mwigizaji bora wa filamu ya El Crimen del Padre Amaro ya nchini Mexiko, mnamo mwaka 2002.

Mnamo mwaka 2003, alipewa tuzo ya Goya kwakuwa mwigizaji bora wa filamu ya 800 balas, ya mwaka 2002. Kwa upande mwingine wa filamu Sancho ameonekana zaidi ya filamu sitini za maonyesho ya nchini Hispania.

Gracia bado anaendelea kujishughulisha na masuala ya ugizaji wa filamu.

Tazama pia hariri

  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sancho Gracia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.