Scientology ni dini mpya iliyoanzishwa na L. Ron Hubbard ili kueneza mitazamo na mbinu za Dianetics aliyoibuni mwaka 1950.

Msalaba wa Scientology.

Lakini inakubaliwa hadhi ya "dini" katika nchi ya Marekani, Australia na nyingine chache, kwa sababu toka mwanzo imehusishwa na makosa mbalimbali ya jinai, hususan ujasusi, utapeli na kuathiri hali ya nafsi ya wafuasi wake.

Kadiri ya hesabu yake, hao mwaka 2005 walikuwa milioni 8, lakini watu wa nje wanakadiria kuwa ni nusu milioni tu.

Makao makuu ya Scientology yako Marekani, katika kijiji cha Clearwater.

Baada ya Hubbard kufariki mwaka 1986, kiongozi mpya ni David Miscavige.

Jina linatokana na neno la Kilatini "scio" (yaani "najua" kwa maana pana), na neno la Kigiriki "logos" (yaani "somo").

Historia

hariri

Historia ya Scientology inaendana kabisa na maisha ya mwanzilishi wake ambaye tangu miaka ya 1930 aliandika vitabu vya ubunifu mkubwa, mpaka alipojingiza katika masuala ya saikolojia akipinga kabisa misingi na maelekeo ya sayansi hiyo.

Kisha kupata umaarufu wa muda mfupi, akaelekea upande wa roho, aliyoiona haitegemei mwili wala akili, ila inavitumia ili kutenda ulimwenguni.

Kuanzia miaka ya 1960 alifukuzwa na nchi mbalimbali na kuhukumiwa na mahakama tofautitofauti.

Uchumi

hariri

Scientology imeitwa "dini ghali" kuliko zote duniani. Kila huduma inatolewa kwa bei iliyopangwa na uongozi wa juu.

Ili kufikia hali ya "Clear", mtu anahitaji kugharimu euro 25.000, na ili kufikia hali bora ya "OT VIII", zinahitajika euro 250,000 hivi.

Viungo vya nje

hariri