Sekwensya (kutoka Kilatini "sequentia", yaani "mwendelezo") ni aina ya wimbo maalumu kwa ajili ya liturujia ya Neno ya Misa ya siku fulani.

Inaimbwa kabla ya Injili.

Historia

hariri

Kifasihi ni mtungo wa kwanza uliotumia vina na ulioandaa mashairi ya baadaye.

Asili yake ni monasteri za Ufaransa katika karne ya 9.

Ingawa mtindo huo ulienea sehemu nyingi, hata kufikia idadi ya 5,000, liturujia ya mapokeo ya Roma haikuukubali sana, na Mtaguso wa Trento katika karne ya 16 uliruhusu 5 tu.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano zimebaki 4 tu: ya Pasaka, ya Pentekoste, ya Mwili na Damu ya Kristo na ya Bikira Maria wa Mateso.

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sekwensya kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.