Selemani Said Jafo
Selemani Said Jafo (amezaliwa 26 Mei 1973) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Kisarawe kwa miaka 2015 – 2020. [1]
Mhe. Selemani Jafo Mb | |
Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi,Muungano na Mazingira
| |
Aliingia ofisini 2017 | |
Rais | John Magufuli |
---|---|
Mbunge wa Kisarawe
| |
Aliingia ofisini 2015 | |
tarehe ya kuzaliwa | 26 Mei 1973 |
utaifa | Mtanzania |
chama | CCM |
Mwaka 2017 alipewa cheo cha waziri katika Ofisi ya Rais kwa ajili ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)[2]. Mnamo tarehe 31 Machi 2021, aliteuliwa na raisi Mama Samia Suluhu Hassan kuwa waziri katika wizara ya ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na mazingira [3] Ameoa wake wanne (4) na wote wako hai.
Elimu
haririSelemani Said Jafo alipata Elimu yake katika shule zifuatazo[4]
Mwaka wa kuanza | Mwaka wa kumaliza | Jina la shule | Ngazi ya Elimu |
---|---|---|---|
2005 | 2007 | Southern New Hampshire University | Shahada ya Uzamili |
1998 | 2001 | Chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine | Shahada ya kwanza |
1995 | 1997 | Shule ya Sekondari ya Minaki | Elimu ya Sekondari |
1991 | 1994 | Shule ya Sekondari ya Maneromango | Elimu ya Sekondari |
1984 | 1990 | Shule ya Msingi ya Kwala | Elimu ya Msingi |
Marejeo
hariri- ↑ Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
- ↑ "Profile | PO-RALG". www.tamisemi.go.tz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-05.
- ↑ https://www.dw.com/sw/mabadiliko-ya-baraza-la-mawaziri-tanzania/a-57066564
- ↑ "Profile | PO-RALG". www.tamisemi.go.tz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-08-05.
Makala hiyo kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |