Septimunicia ilikuwa mji wa Dola la Roma katika jimbo la Kiroma la Afrika ya Kiroma na baadaye Jimbo la Byzacena. Mahali pake kamili hapajathibitishwa bado, pakitafutwa katika magofu ya Oglet-El-Metnem au Henchir-El-Bliaa katika Tunisia ya leo.

Dola la Rumi kaskazini mwa Afrika (125 BK)

Septimunicia ilikuwa makao ya askofu aliyetajwa mnamo mwaka 484. Kanisa Katoliki limeanza kutumia tena jina la dayosisi hiyo baada ya mwaka 1933 kama dayosisi ya cheo kwa ajili ya maaskofu wasio na dayosisi hai.[1][2] Hamna uhakika wa mahali ilipo, ila inadhaniawa kuwa ipo Tunisia.

Marejeo hariri

  1. Pius Bonifacius Gams, Series episcoporum Ecclesiae Catholicae, (Leipzig, 1931), p. 468.
  2. Stefano Antonio Morcelli, Africa christiana, Volume I, (Brescia, 1816), p. 274.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Septimunicia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.