Sera ya nishati ni namna ambavyo chombo husika (mara nyingi serikali) kimeamua kushughulikia masuala ya maendeleo ya nishati ikiwa ni pamoja na ubadilishaji wa nishati, usambazaji, matumizi pamoja na kupunguza uzalishaji wa gesi chafu ili kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Sifa za sera ya nishati zinaweza kujumuisha sheria, mikataba ya kimataifa, motisha kwa uwekezaji, miongozo ya uhifadhi wa nishati, ushuru na mbinu zingine za sera za umma.nishati ni sehemu muhimu ya uchumi wa kisasa. Uchumi unaofanya kazi hauhitaji tu kazi na mtaji bali huitaji pia nishati, kwa michakato ya utengenezaji, usafirishaji, mawasiliano, kilimo, na zaidi. Upangaji wa nishati ni wa kina zaidi kuliko sera ya nishati.[1]

Marejeo hariri