Sergio Sollima (amezaliwa tar. 27 Aprili 1921 mjini Roma) ni mwongozaji na mtunzii wa filamu wa zamani kutoka nchini Italia.

Sollima alianza kuongoza filamu nyingi sana za mtindo wa sword na sandal ambazo zilitamba sana katika miaka ya 1960. Pamoja na kuvuma sana kwa mtindo huo wa sword na sanda, baadae ulikuja kufa kabisaa ukawa hauna wapenzi kama ilivyokuwa awali. Kitendo hicho kilipelekea Sollima kuwa miongoni mwa waongozaji wa filamu wa kwanza kukimbilia katika filamu za western ya Italia, maarufu kama Spaghetti Western.

Akiwa huko aliongoza filamu ya The Big Gundown (alicheza nyota Lee van Cleef na Tomas Milian) filamu ilitolewa mnamo mwaka wa 1966 ikiwa imepata mafanikio makubwa kabisa, licha ya ukweli uliopo filamu iliweza kushindana kidogo na filamu zilioongozwa na Sergio Leone The Good, the Bad and the Ugly na vile vile za mwongozaji Sergio Corbucci Django.

Baadae kidogo Sollima akatengeneza filamu zingine mbili za western, Face to Face (nyota alikuwa Milian na Gian Maria Volonté) filamu ilitolewa mnamo mwaka 1967, kisha akatoa Run, Man, Run! (nyota alikuwa tena Milian) mnamo mwaka wa 1968. Japokuwa Sollima aliongoza filamu tatu za westerns lakini vile vile hakufikia usawa ule wa filamu maarufu kama za waongozaji (Leone na Corbucci), kila mmoja katika hao wamekuwa miongoni mwa waongozaji wa filamu waliopata washabiki wengi wengi kuliko waongozaji wote wa filamu za western.

Filamu alizoongoza Sollima hariri

  • The Big Gundown (1966)
  • Face to Face (1967)
  • Run, Man, Run! (1968)
  • Violent City (1970)
  • Revolver (1973)
  • Sandokan (1976)

Ona pia hariri

Viungo vya nje hariri