Zabibu ni tunda la mzabibu (Vitis vinifera).

Zabibu
Shamba la mizabibu

Zabibu moja ni fuu inakua pamoja na fuu nyingine 6 - 300 kwenye mshikano au shazi kama ndizi. Zabibu hupatikana kwa rangi mbalimbali hasa kijani, njano, buluu, nyeusi na namna za nyekundu.

Zabibu zinajulikana hasa kama chanzo cha divai lakini huliwa kama tunda, hufanywa kuwa maji ya zabibu, kuwa jem au kukaushwa kuwa zabibu kavu. Mbegu zake ndogo hutoa mafuta.

Zabibu

Utangulizi

hariri

Mzabibu ni mmea wa jenasi Vitis; uliokuwa muhimu katika mabadiliko ya maisha ya mwanadamu, kitaalamu tunda dogo, linalolimwa kwa miaka zaidi na kupukutisha majani. Zabibu huweza kuliwa mbichi au zikatumika kutengenezea jemu, sharubati, jeli, siki, madawa, mvinyo, zabibu kavu na mafuta ya mbegu zake. Zabibu pia hutumika kutengenezea vitu vitamuvitamu. Zabibu wakati mwingine hutumika kama alama ya dhamiri.

Historia

hariri

Kilimo cha zabibu kilianza mahali kunapofahamika sasa kama Uturuki. Hamira, moja ya vidubini waliofahamika mapema zaidi, hupatikana kiasili kwenye ngozi ya zabibu, na kupelekea kugunduliwa kwa vileo kama vile mvinyo. Kibiblia tunda hili ni tunda lililokwa limelimwa zamani sana na ilivyo kwenye Biblia inasema kwamba Noah alikuwa mkulima wa kwanza baada ya janga la mvua kubwa na alikuwa ni mkulima wa zabibu. Kumbukumbu za kihistoria za huko Misri zinaonesha kilimo cha zabibu, na hata zamani ya Ugiriki, Fenisia na Roma pia walilima zabibu kwa ajili ya kula na kutengeneza mvinyo. Baadae, kilimo cha zabibu kilisambaa mpaka Ulaya, kaskazini mwa Afrika, na hatimaye mpaka Amerika ya kaskazini.

Zabibu za asili ni zile za jenasi Vitis iliyoenea upesi maeneo ya Amerika ya kaskazini, na ilikuwa sehemu ya mlo kwa watu wengi wa mwanzo wa Amerika ya Kaskazini, lakini ilionwa na wakoloni kutoka Uingereza kuwa hazifai kwa kutengeneza mvinyo. Zabibu za Dunia ya Kale, vitis vinifera zililimwa huko Kalifornia ambako Wahispania walianzisha msululu wa monasteri kwenye fukwe kwaajili ya wanajeshi wao na machungwa tele kuwakinga na ugonjwa na ngozi kiseyeye na kwabadilisha wazawa.

Maelezo

hariri
 
Kichana cha zabibu

Zabibu hukua kwenye kichana chenye zabibu 6 mpaka 300, na huweza kuwa za rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza, njano, kijani na hata pinki. Zabibu “nyeupe” huwa na rangi ya kijani hasa, na kiasili hutokana na zabibu nyekundu. Kubadilika hukukwa kizazi hutokana na zabibu kukata uzalishaji wa pigmenti ya anthocyanins ambazo huwa na jukumu la kuzipa rangi zabibu. Pigmenti hii ya anthocyanins na nyingine kadhaa za familia ya ‘polyphenols’ kwenye zabibu nyekundu na huhusika na kubadilisha kivuli kwenye mvinyo mwekundu.

Mizabibu

hariri

Zabibu nyingi hutokana na mazao ya Vitis vinifera, zabibu ya Ulaya yenye asili ya Mediteranea na Asia ya Kati. Kiasi kidogo cha zabibu na mvinyo hutokana na spishi za Amerika na Asia:

  • Vitis labrusca, sharubati ya mezani na mizabibu ya huko Amerika ya Kaskazini ( hujumuisha aina kali ), na wakati mwingine hutengenezea mvinyo. Asili yake ni Marekani mashariki na Kanada.
  • Vitis riparia, mzabibu mwitu wa Amerika ya kaskazini, wakati mwingine hutumika kutengenezea mvinyo na jemu. Asili yake ni Marekani mashariki na Kubeki kaskazini.
  • Vitis rotundifolia, hutumika kwa mvinyo na jemu. Asili yake ni Marekani kusini-mashariki kutoka Deleware mpaka Ghuba ya Mexico.
  • Vitis amurensis, spishi muhimu ya Asia.

Mgawanyiko na uzalishaji

hariri

Kulingana na shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo, ( FAO ), kilometa za mraba za dunia zinatumika kwa kilimo cha zabibu. Asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengeneza mvinyo, 27% huliwa kama matunda ya kawaida na 2% kama zabibu za kukausha. Maeneo haya yaliyotengwa kwa kilimo cha zabibu hukua kwa 2% kila mwaka. Jedwali lifuatalo linaonesha wazalishaji wakubwa wa mvyinyo na maeneo ya nchi hizo yaliyotengwa kwa kilimo cha zabibu.

Zabibu zisizo na mbegu

hariri

Kutokuwa na mbegu ni ubora wa zabibu unaohitajika katika uchaguzi wa zabibu, na zabibu zisizo na mbegu sasa huchukua asilimia kubwa ya zabibu kwaajili ya kuliwa na watu. Kwasababu mizabibu hupandwa kwa vipandikizi, kukosekana kwa mbegu hakuna matatizo yeyoye kwa wakulima. Huwa tatizo tu kwa wakulima ambao wanataka aidha kutumia mbegu kuhifadhi kizazi husika au kama wanataka kufanya mabadiliko katika hatua za mwanzo za kiini kwa kutumia tishu kwa kutumia mbinu za ukuzaji wa bakteria.

Kuna vyanzo kadhaa vya zabibu zisizo na mbegu, na kimsingi mazao yote ya kibiashara yametokana na vyanzo vikuu vitatu: Thompson Seedless, Russian Seedless, na Black Monukka, aina zote hizi zikiwa ni za spishi ya Vitis vinifera. Hivi sasa kuna zabibu zisizo na mbegu nyingi kiasi, kama vile Einset Seedless, Reliance na Venus, zimekuwa zikilimwa kwa ajili ya ugumu na kwa wastani kuwa baridi kwenye maeneo ya baridi ya kaskazini mashariki ya marekani na kusini mwa Ontario. Fidia ya kuwa na kula zabibu hizi za hali ya juu ni kukosa faida lukuki muhimu zinazotokana na kemikali zenye virutubisho tele zilizopo kwenye mbegu za zabibu.

Zabibu za kukaushwa

hariri
 

Zabibu huliwa pia zikiwa zimekaushwa, kuongeza pia uwezo wa kustahimili kukaa kwa muda mrefu. Huko Ulaya, zabibu za kukaushwa huitwa ‘raisins’ au kwa lugha nyingine za asili. Na huko Uingereza kuna aina tatu za zabibu za kukaushwa na hii ililazimisha mamlaka kutumia msamiati “ mazao ya kukaushwa ya mzabibu” kwenye nyaraka za kiofisi. “Raisin” ni zabibu yeyote ya kukaushwa. Huku neno raisin likiazimwa kutoka kwene lugha ya kifaransa, katika kifaransa neno hili humaanisha zabibu mbichi za kawaida. Kifaransa ‘grape’ (ambapo katika kiingereza huwa ‘grape’ na Kiswahili ‘zabibu’) “Currant” hukaushwa kutokana na zabibu za Zante Black Corinth, jina lilochukuliwa tena kutokana na lugha ya kifaransa, raisin de Corinthe ( zabibu za Corinth ). Tambua pia kuwa Currant imekuja kuwa na maana ya blackcurrant na redcurrant, matunda yasiyohusianan na zabibu kabisa.

“Sultana” kiasili ni raisin iliyotengenezwa kutokana na aina maalumu ta zabibu kutoka Uturuki, lakini dunia sasa inatumia msamiati huu kumaanisha raisins zilizotengenezwa kwa zabibu za kawaida na kutengenezwa zifanane na sultana ya kweli. Masuala ya Afya.

Fumbo la Ufaransa

hariri

Ukilinganisha na nchi nyingine za magharibi, watafiti wamegundua kuwa japokiwa Wafaransa hula kiasi kikubwa cha mafuta, inashangaza kuwa kiasi cha maradhi ya moyo kinabakia kuwa ni kidogo huko Ufaransa, suala linalofahamika kama Fumbo la Ufaransa na hufikiriwa kuwa linatokana na faida za kinga kutokana na maatumizi ya mara kwa mara ya mvinyo mwekundu. Mbali na faida za kilevi chenyewe, ikijumuishwa na kuongezeka kwa chembe sahani za damu na kutanuka na kusinyaa kwa mishipa ya damu, polyphenols ( kama vile resveratol ) hasa kwenye ngozi ya zabibu, hutuoa faida nyingine za kiafya, kama vile; kubadilika kwa ufanyaji kazi wa molekyuli za damu katika mishipa ya damu, kupunguza hatari ya kuharibika kwa mishipa ya damu.

Kupungua kufanya kazi kwa angiotensin, homoni inayosababisha mishipa ya damu kusinyaa hali ambayo ingaesababisha kupanda kwa mgandamizo wa damu.

Huongeza uzalishaji wa homoni ya vasodilator, na naitriki oksaidi. Ingawa mataumizi ya mvinyo hayashauriwi na baadhi ya mamlaka fulani za afya, tafiti nyigni za kuaminika zimeonesha kuwa unywaji kiasi wa mvinyo, kama vile glasi moja ya mvinyo mwekundu kwa siku kwa wanawake na mbili kwa wanaume, hupelekea ayfa bora. Tafiti mpya zinaonesha kuwa kemikali za polyphenols za mvinyo kama vile reseveratrol huleta faida za kisaikolojia huku kilevi chenyewe kikiwa na faida pia kwenye mfumo wa mzungukok wa damu.

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zabibu kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.