Shankar Mahadevan (amezaliwa 3 Machi 1967) ni mwimbaji na mtunzi wa Kihindi ambaye ni mmoja wa waimbaji katika kundi la Trio ya Shankar-Ehsaan-Loy wanaoandika muziki kwa ajili ya filamu za Kihindi.

Shankar Mahadevan

Maisha ya awali hariri

Shankar Mahadevan alizaliwa huko Chembur, Mumbai katika familia inayoongea lugha Kitamil huko Palakkad, Kerala. Alijifunza muziki wa Hindustani na Carnatic akiwa mtoto na alianza kucheza veena akiwa na umri wa miaka mitano akifundishwa na Shri Lalitha Venkataraman. Mahadevan alifundishwa muziki na Pandit Shrinivas Khale na T.R. Balamani. Alihitimu shahada ya Sayansi ya Kompyuta na Uhandisi wa Programu kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Ramano Adik huko Navi Mumbai mnamo 1988. Siddharth Mahadevan ni mtoto wa Shankar Mahadevan na pia ni mwimbaji.[1][2][3][4]

Marejeo hariri

  1. "Khale a maestro till his last breath: Mahadevan". yahoo.com. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-23. Iliwekwa mnamo 2023-04-10.  More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help)
  2. "Best Marathi songs by Shankar Mahadevan you would love to listen to", Times of India., 5 October 2018. 
  3. Ramani, Hema Iyer Ramani and V. v. "The sound of his music", The Hindu, 2017-07-27. (en-IN) 
  4. "Shankar Mahadevan Biography". Filmi Beat. Iliwekwa mnamo 18 February 2013.  Check date values in: |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shankar Mahadevan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.