Shinyanga (mji)
Shinyanga ni manisipaa nchini Tanzania ambayo ni makao makuu ya Mkoa wa Shinyanga yenye msimbo wa posta 37100. Manisipaa ya Shinyanga ni sawa na Wilaya ya Shinyanga Mjini.
Manisipaa ya Shinyanga | |
Mahali pa mji wa Shinyanga katika Tanzania |
|
Majiranukta: 3°39′36″S 33°25′12″E / 3.66000°S 33.42000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Shinyanga |
Wilaya | Shinyanga Mjini |
Eneo
haririManispaa ya Shinyanga ina eneo la km² 548. Eneo la utawala linaundwa na jumla ya tarafa 3, kata 17,vijiji 19, mitaa 25 na vitongoji 95.
Wakazi
haririKulingana na sensa ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 161,391 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 214,744 [2].
Halihewa
haririHali ya hewa ni ya kitropiki ambayo ina vipindi viwili ya majira ya mvua na kiangazi. Msimu wa mvua ni kati ya mwezi Oktoba na Desemba,pia huanza mwezi machi hadi Mei. Kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya milimita 600 hadi 1000. Kiangazi huanza mwezi Mei hadi Oktoba, pia huanza Januari hadi Februari. Wastani wa jotoridi ni kati ya nyuzi za sentigredi 18 hadi 31.[3]
Usafiri
haririShinyanga huwa na kituo cha reli kwenye njia ya reli kutoka Mwanza kwenda Tabora; kwa hiyo imeunganishwa na reli ya kati Dar es Salaam - Tabora - Kigoma. Kuna uwanja wa ndege mdogo. Mji unapitiwa na barabara ya lami kutoka Mwanza kwenda Tabora.
Utamaduni
haririWakazi wengi hupendelea ngoma za asili pamoja na michezo ya mbio za baiskeli, kwani ndio utamaduni wa wasukuma.
Pia, Shinyanga ni moja ya mikoa ambayo vijana wengi wako katika mrengo wa muziki wa Hip Hop, wengi wao wakifanya harakati tofauti kwa ajili ya ukombozi.
Kati ya wanamuziki maarufu wapo Noorah, Ibrah Mpanduji, na Big.com ambao wote wanafanya mahadhi ya Hip Hop.
Marejeo
hariri- ↑ Sensa ya 2012, Shinyanga Region - Shinyanga Municipal Council
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Maelezo kuhusu hali ya hewa kutoka tovuti ya manisipaa , ilitazamiwa Septemba 2015
Viungo vya Nje
hariri- Tovuti rasmi ya Manisipaa ya Shinyanga
- Makisio ya Halmashauri ya manisipaa ya Shinyanga kwa mwaka 2011-12 Ilihifadhiwa 17 Aprili 2016 kwenye Wayback Machine.
Kata za Wilaya ya Shinyanga mjini - Mkoa wa Shinyanga - Tanzania | ||
---|---|---|
Chamaguha | Chibe | Ibadakuli | Ibinzamata | Kambarage | Kitangili | Kizumbi | Kolandoto | Lubaga | Masekelo | Mjini | Mwamalili | Mwawaza | Ndala | Ndembezi | Ngokolo | Old Shinyanga |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Shinyanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Shinyanga (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |