Simon Abkarian
Simon Abkarian (amezaliwa 5 Machi 1962) ni mwigizaji wa filamu wa Ufaransa.
Simon Abkarian |
---|
Amezaliwa katika mji wa Gonesse, Val d'Oise kutoka ukoo wenye asili ya Armenia. Abkarian alikulia utoto wake nchini Lebanon. Yeye alihamia jijini Los Angeles, ambako alijiunga na kampuni ya uigizaji ya Armenien theater company iliyosimamiwa na Gerald Papazian. Yeye alirudi Ufaransa mwaka 1985, na kuishi mjini Paris.
Amewahi kuigiza katika filamu takriban thelathini, akipata umashuhuri kwenye filamu ya Atom Egoyan iitwayo Ararat, na Yes, ambapo yeye aliigiza kwenye nafasi ya kuongoza. Abkarian aliigiza kama adui kwa jina Alex Dimitrios katika filamu ya James Bond inayoitwa Casino Royale. Alikuwa anaigiza kama mfanyikazi wa serikali na muuzaji silaha anayempinga Bond.
Yeye anapaswa kuigiza katika nafasi ya muigizaji mkuu kwenye filamu ya La Bombe humaine (Binadamu aliye Bomu), filamu ambayo ni ya kisiasa, iliyoandikwa na Laurent Touil-Tartour, iliyorikodiwa kwa kamera mwaka 2007. Yeye pia ameigiza kama Dariush Bakhshi, ambaye ni Mtaalam wa kutoka Iran, katika maigizo ya BBC ya Spooks.
Filamu
hariri- Ararat (2002), Arshile Gorky
- The Truth about Charlie (2002), Lieutanant Dessalines
- Aram (2002), Aram
- Yes (2004), He
- Le Voyage sw Arménie (2006), Sarkis Arabian
- Casino Royale (2006), Alex Dimitrios
- Persepolis (2007), Mr Satrapi - babake Marjane (sauti)
- Rendition (2007), Said Abdel Aziz
- Rage (2009), Merlin
- The Army of Crime (2009)
Viungo vya nje
hariri- Simon Abkarian at the Internet Movie Database
- Brief biography katika Kifaransa
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Simon Abkarian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |