Simon Kimbangu

Simon Kimbangu (12 Septemba 1887 - 12 Oktoba 1951) alikuwa mwinjilisti wa Kibaptisti Kongo ya Kibelgiji aliyeonekana kuwa na karama ya uponyaji.Watu wengi walimwendea kutafuta nafuu wakasikia mahubiri yake

Simon Kimbangu (12 Septemba 1887 - 12 Oktoba 1951) alikuwa mwinjilisti wa Kibaptisti Kongo ya Kibelgiji aliyeonekana kuwa na karama ya uponyaji.

Washiriki wa Kanisa la Kimbangu la Ureno wakisherehekea Mwaka Mpya Mei 25, 2013 nje ya Lisbon, Ureno.

Watu wengi walimwendea kutafuta nafuu wakasikia mahubiri yake, lakini serikali ya kikoloni ya Ubelgiji iliogopa mikutano mikubwa ya Waafrika bila usimamizi wa Wazungu au machifu.

Hivyo Kimbangu akaagizwa na wamisionari kwa amri ya serikali aache mahubiri na uponyaji lakini hakuweza kutii.

Wabelgiji wakamkamata wakamfunga gerezani miaka mingi mpaka kifo. Kabla hajafa alimuomba sista aliyemuuguza ambatize Kikatoliki akakubaliwa kwa kupewa ubatizo wa sharti.

Wafuasi wake wakamwamini kuwa nabii wa Mungu, wengine walisema ndiye Yesu aliyerudi, wakatoka katika uongozi wa wamisionari walionyamaza mbele ya tendo la serikali la kumfunga Kimbangu bila kosa.

Kati ya wafuasi wake limetokea "Kanisa la Kristo kwa Mtume wake Simon Kimbangu" ambalo leo lina waumini milioni kadhaa katika nchi kadhaa.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.