Simone Deveaux
Simone Deveaux ni jina la kutaja uhusika wa tamhilia ya ubunifu wa kisayansi ya Heroes. Uhusika umechezwa na Tawny Cypress.
Simone Deveaux | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Mwonekano wa kwanza | "Genesis" |
Mwonekano wa mwisho | "How to Stop an Exploding Man" |
Imechezwa na | Tawny Cypress |
Maelezo | |
Kazi yake | Mwuza Michoro ya Sanaa |
Historia ya uhusika
haririGenesis
haririWakati Simone Deveaux anatambulishwa katika sehemu ya kwanza, yeye ni mwuza michoro anayeishi mjini New York City ambaye ana-mahusiano ya kimapenzi na msanii Isaac Mendez. Hata hivyo, lakini amekuwa akikerekwa sana uzoezi wa matumizi mabaya ya heroini yanayofanywa na Isaac na kujidai kwamba akitumia dawa hizo ndipo anakuwa na uwezo wa kuchora matukio ya baadaye.
Kwenye kipengele cha "One Giant Leap", Simone anachukua mchoro wa Claire na Zach na kumweleza Isaac kwamba anaenda kuziuza picha zile na kisha aende kufanyiwa uondolewaji wa matumizi mabaya ya dawa za kulevya. Wakati Isaac anakataa, akaachana naye. Siku ile baadaye, Peter Petrelli, ambaye hivi karibuni amekuwa akimwuguza baba wa Simone, amekiri penzi lake kwa Simone. Ijapokuwa wawili hao walitumia pamoja usiku wao, lakini bado Simone hataki kuwa na pupa ya mahusiano mapya.
Siku kadhaa badaye, Simone anamweleza Peter kwamba baba yake amefariki. Wakati Peter anaulizia picha zilizochorwa na Isaac ambazo zimeuzwa karibuni na Simone, Simone anamweleza kwamba zimenunuliwa na Mr. Linderman.
Baada ya ndugu wa Peter, Nathan, amezipata zile picha, yeye na Simone wakazifungua pamoja. Nathan akazichana-chana zile picha, kitendo ambacho kimemkera Simone. Hata hivyo, amekuwa na uwezo wa kumwonesha Peter nakala ya dijitali na picha imeonesha kuna mtu kafa lakini anafanana na Peter. Pamoja na hayo, Peter anaamua kwenye katika shule ya Union Wells na kwenda kumwokoa Homecoming aliyeonekana katika picha. Simone akaanza kuamini kwamba Isaac anaweza kuchora matukio ya baadaye, na kuamini kwamba Peter atarudi salama.