Julai

mwezi wa saba katika mwaka
Jun - Julai - Ago
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30 31
Kalenda ya Gregori

Mwezi wa Julai ni mwezi wa saba katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na jina la Julius Caesar wa Warumi (angalia pia Kalenda ya Juliasi). Kwa asili, mwezi huo wa Julai ulikuwa mwezi wa tano katika kalenda ya Warumi, na jina lake lilikuwa Quintilis kulingana na neno la Kilatini quintus, maana yake ni "wa tano". Mwaka wa 153 KK, mwanzo wa mwaka ulitanguliza miezi miwili kutoka Machi kwenda Januari, na maana ya jina Quintilis ilipotea. Mwaka wa 44 KK, Quintilis ilibadilika kuitwa Julai (kwa Kilatini Julii).

Julai ina siku 31, na inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Aprili; na katika mwaka mrefu (wenye siku 366), siku yake ya kwanza pia ni sawa na mwezi wa Januari.

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: