Sophia Mattayo Simba

Sophia Mattayo Simba (alizaliwa tarehe 27 Julai 1950) ni mwanasiasa wa chama cha Mapinduzi kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge kwenye viti maalum vya wanawake kwa chama cha CCM. Mwaka 2015 alirudishwa bungeni[1]. Alikuwa pia mwenyekiti wa kitaifa wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania na waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Mwezi wa Machi 2017 alifukuzwa katika chama cha CCM[2] hivyo alitoka pia katika vyeo vyake vya siasa pamoja na nafasi yake bungeni.

Marejeo

hariri
  1. Hon. Sophia Mattayo Simba
  2. CCM yamfukuza uanachama Sophia Simba, tovuto ya VOA, iliangaliwa Juni 2017