South Georgia ni funguvisiwa muhimu zaidi katika eneo la ng'ambo la Uingereza kusini mwa Bahari Atlantiki linaloitwa "Visiwa vya South Georgia na South Sandwich".

Makazi ya zamani kwenye kisiwa cha South Georgia pamoja na kijiji hai cha Grytviken

Idadi ya wakazi ni 20 na wengi wao ni wanasayansi wanaochungulia ndege wanaokaa kwenye visiwa pamoja na afisa mmoja mwakilishi wa serikali ya Uingereza.

Wakazi hariri

Hakuna wenyeji kwenye visiwa hivi. Tangu karne ya 19 wavuvi wa nyangumi kutoka Ulaya walijenga huk vituo ambako walipeleka nyangumi kwa kuwakatakata na kupika mafuta yao. Vituo hivyo vilikuwa na makumi hadi mamia ya wakazi wakati wa kuwinda nyangumi lakini wakati wa baridi ni watu wachache tu waliobaki. Vituo hivyo vilifungwa katika miaka ya 1960 kutokana na kupotea kwa nyangumi.

Mwaka 1904 mvuvi kutoka Norwei alianzisha kijiji cha Grytviken kama kituo cha kupikia mafuta ya nyangumi na kijiji hicho ni makazi pekee ya kudumu kwenye visiwa hivi hadi leo.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.