Eneo la ng'ambo la Uingereza

Eneo la ng'ambo la Uingereza ni moja kati ya maeneo 14 ambayo ni chini ya serikali ya Uingereza lakini si sehemu za nchi.

Ramani ya maeneo ya ng'ambo ya Uingereza
(Eneo la Kiingereza kwenye Antaktika na Akrotiri na Dhekelia (Kupro) havionyeshwi)

Kwa Kiingereza yameitwa "British Overseas Territory" tangu sheria ya 2002 badala ya jina la awali "British dependent territory" yalivyoitwa tangu 1981. Kabla ya 1981 yaliitwa "koloni"

Hali ya maeneo haya ni tofauti na Jumuiya ya Madola ambayo ni jumuiya ya hiari ya koloni za zamani za Uingereza.

Mambo ya kisheriaEdit

Kwa jumla wakazi wa maeneo ya ng'ambo ya Uingereza ni raia wa Uingereza wana haki kuhamia Uingereza penyewe. Kila eneo lina bunge lake na uhuru fulani wa kutunga sheria zake.

Visiwa vya mfereji wa Kiingereza (Jersey, Guernsey) na Isle of Man si maeneo ya ng'ambo ya Uingereza bali "maeneo chini ya taji la Uingereza".

Maeneo ya ng'ambo ya UingerezaEdit

Bendera Eneo Mahali Wito Eneo Wakazi Mji Mkuu
  Anguilla Karibi Strength and Endurance 102 km²
(39.4 mi²)
12,8 The Valley
  Bermuda Atlantiki Quo fata ferunt (Kilatini: "Pote heri inapotupeleka") 53.3 km²
(20.6 mi²)
64,482 Hamilton
  Eneo la Uingereza katika Antaktika Antarctica Research and discovery 1,709,400 km²
(666,000 mi²)
200 staff Rothera (kituo kikuu)
  Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi Bahari Hindi In tutela nostra Limuria (Kilatini: "Tumekabidhiwa Limuria") 60 km²
(23 mi²)
3,200 military and staff Diego Garcia (kituo cha kijeshi)
  Visiwa vya Virgin vya Uingereza Karibi Vigilate (Kilatini: "Mwe macho!") 153 km²
(59 mi²)
21,73 Road Town
  Visiwa vya Cayman Karibi He hath founded it upon the seas 260 km²
(100.4 mi²)
57,8 George Town
  Visiwa vya Falkland Atlantiki Desire the right 12,173 km²
(4,702 mi²)
2,967 Stanley
Gibraltar Ulaya ya Kusini Nulli expugnabilis hosti (Kilatini: "Haishindwi na adui yeyote") 6.5 km²
(2.5 mi²)
27,776 Gibraltar
  Montserrat Karibi 102 km²
(39 mi²)
9 Plymouth
  Visiwa vya Pitcairn Pasifiki 43 km²
(17 mi²)
(all islands)
67 Adamstown
  Saint Helena (pamoja na Ascension na Tristan da Cunha)   Atlantiki Loyal and unshakeable 410 km²
(158 mi²)
(all islands)
6,563 Jamestown
  Visiwa vya South Georgia na South Sandwich Atlantiki Leo terram propriam protegat (Kilatini: "Simba alinda kwake") 3,903 km²
(1508 mi²)
11-26 staff King Edward Point/Grytviken
  Akrotiri and Dhekelia (Kupro) Mediteraneo (Kupro) Dieu et mon droit (Kifaransa: "Mungu na haki yangu") 254 km²
(98 mi²)
wanajeshi 15,000 Episkopi Cantonment
  Visiwa vya Turks na Caicos Karibi One people, one nation, one destiny 430 km²
(166 mi²)
26,288 Cockburn Town

Viungo vya NjeEdit